Thursday, November 29, 2012

GAUDENCE KAYOMBO AWATAKA WANANCHI WAKE KUJITUMA KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO


Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

WANANCHI wa jimbo la Mbinga Mashariki mkoani Ruvuma, wametakiwa kuendelea kujituma katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili waweze kuondokana na umaskini, ambao umekuwa ukiitesa jamii miongoni mwao.

Mbunge wa jimbo hilo Bw. Gaudence Kayombo(Pichani) alisema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, juu ya mikakati mbalimbali ya kusukuma maendeleo katika jimbo lake.

Bw. Kayombo alisema kuwa anafurahishwa na wananchi wa jimbo la Mbinga Mashariki, kwamba wengi wao wamekuwa wakijituma katika shughuli za maendeleo hasa katika nyanja ya kilimo cha mazao mbalimbali.

Wednesday, November 28, 2012

BALOZI ALITOA TAARIFA ZA KUPOTOSHA

BALOZI wa Marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice amekiri kwamba alitoa habari zisizokuwa sahihi, kufuatia shambulio lililotekelezwa dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani nchini Libya mwezi Septemba.

Shambulio hilo lilisababisha kifo cha balozi wa marekani nchini Libya Christopher Stevens.

WAPINGA JESHI KUWAZUIA WANAWAKE MAREKANI

CHAMA cha kupigania haki za kiraia nchini Marekani kimewasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi wa jeshi la taifa hilo, kuwapiga marufuku wanajeshi wa kike kufanya kazi katika maeneo ya vita.

Chama hicho ambacho kiliwasilisha kesi hiyo kwa niaba ya wanajeshi wanne wa kike kinasema sera hiyo inakiuka katiba.

Kundi hilo linasema licha ya hatua ya kulegeza sera hiyo katika miaka ya hivi karibuni, wanawake bado wananyimwa fursa ya kuhudumu katika nyadhfa zaidi ya mia mbili vitani katika jeshi la Marekani.

WAKAMATWA KWA PESA HARAMU

WAZIRI wa mambo ya ndani wa Bolivia, Carlos Romero amesema, kuwa maafisa kadhaa wa serikali wametiwa mbaroni kwa kujaribu kupokea pesa kutoka kwa mfanyibiashara mmoja kutoka Marekani ambaye anahudumia kifungo cha jela nchini humo.

Wale waliokamatwa ni pamoja na Mkurugenzi wa maswala ya kisheria katika wizara ya mambo ya ndani Fernando Rivera.

WAANDAMANAJI WAKESHA KUMPINGA RAIS

Rais Mursi wa Misri anapingwa kwa kujilimbikizia madaraka












WAANDAMANAJI wamekesha usiku kucha katika medani ya Tahrir mjini Cairo kuelezea hasira zao dhidi ya tangazo la rais wao anayezingatia itikadi za kiislamu Mohammed Morsi kujipatia madaraka makubwa.

Walikesha wakiimba nyimbo za kumlaani rais pamoja na vuguvugu lake la kiislamu la Muslim Brotherhood.
Jana Jumanne, maelfu ya waandamanaji walifurika katika medani hiyo wakiandaa mandamano kadhaa huku wakisema watamkiuka rais Mursi huku wakipinga mamlaka aliyojilimbikizia.

TUNDURU WAITAKA SERIKALI KUWABANA VIONGOZI WASIOWAJIBIKA IPASAVYO


Na Steven Augustino,
Tunduru.

BAADHI ya wakulima wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wameitaka serikali kuwabana viongozi wenye tabia ya kujinufaisha matumbo yao kupitia pembejeo za ruzuku ili wananchi waweze kuboresha mashamba yao katika msimu huu wa kilimo.

Hayo yalisemwa na wadau mbalimbali waliohudhuria katika mdahalo wa kukusanya maoni kupitia mdahalo wa kuwajengea uwezo juu ya utekelezaji wa shughuli za sekta ya kilimo uliowahusisha wadau wa kilimo kutoka jimbo la Tunduru Kaskazini uliofanyika ukumbi wa Skyway mjini hapa.

Kadhalika wakulima hao   walishauri kwamba serikali iangalie uwezekano wa kuondoa utaratibu wa kupeleka pembejeo hizo kwa wakulima wake na badala yake  ihamasishe wawekezaji kujenga viwanda vingi ili kuongeza uzalishaji na fedha hizo kuingizwa kama hisa katika viwanda hivyo ili mbolea au mbegu ziuzwe kwa bei nafuu.

Wakifafanua wakati wa kuchangia maoni yao kwa nyakati tofauti Bw. Sekula Matumla, Bw. Addo Makanya, Rashid Issaya, Halifa Chitemwe na Bi. Sarra Mwingira walisema kuwa hali hiyo inatokana na viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo wakiwemo wawakilishi wao madiwani na wabunge, kutokuwa na mwamko wa kusimamia kikamilifu ugawaji wa pembejeo za ruzuku zinazotolewa na serikali.

Tuesday, November 27, 2012

TAARIFA YA KIFO CHA SHARO MILIONEA HII HAPA

Sharo Milionea afariki dunia mkoani Tanga.

















Msanii na mwigizaji maarufu nchini Tanzania Sharo Milionea amefariki dunia leo saa 2:00 usiku mkoani Tanga kwa ajali ya gari.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga, amesema kwamba msanii hiyo amepata ajali saa 2:00 usiku tarehe 26, Novemba, 2012.

“Leo majira ya saa 2:00 usiku kwenye Barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza,


"alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza, gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”, amesema Kamanda huyo.

Monday, November 26, 2012

HALMASHAURI YATENGA BAJETI YA SHILINGI MILIONI 40 KWA MIRADI YA KILIMO

Na Dustan Ndunguru,
Songea.
HALMASHAURI ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, imetenga kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kilimo katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2013.

Mwenyekiti wa kamati ya uchumi ujenzi na mazingira Bw. Teofanes Mlelwa, alisema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu, juu ya utekelezaji wa miradi ya DADPS katika kipindi hicho.

Bw. Mlelwa ambaye pia ni diwani wa kata ya Wino Songea vijijini,  alivitaja vijiji vitakavyonufaika na fedha za mradi huo wa maendeleo ni Mpandangindo, Matimira ambavyo vitalima zao la alizeti, Wino na Lilondo na Liganga vitajikita katika kilimo cha zao la kahawa, ambapo vijiji vya Muhukuru Nakawale na Ngadinda vyenyewe vitashughulika na kilimo cha zao la korosho na kwamba kijiji cha Magingo kitajihusisha na kilimo cha zao la Tangawizi ifikapo June 2013.

SERIKALI MKOANI RUVUMA KUMUONDOLEA UVIVU MKANDARASI WA BARABARA YA NAMTUMBO TUNDURU



Na Steven Augustino,

Songea.


SERIKALI mkoani Ruvuma imesema, imefikia mwisho wa kuendelea kumvumilia mkandarasi anayejenga barabara kwa kiwango cha lami, kutoka wilaya ya Namtumbo kwenda Tunduru mkoani humo, yenye urefu wa kilometa 192 kwa madai kuwa ameshindwa kazi na ujenzi wake haukidhi viwango vinavyotakiwa.



Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu amesema hayo na kuitaja kampuni hiyo kuwa ni ya Progressive Higleig Jv Contractors.

WAFANYABIASHARA WAJERUHIWA NA MAJAMBAZI TUNDURU



Na Steven Augustino,
Tunduru.

WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemvamia mfanyabiashara mmoja anayenunua mpunga na kujeruhiwa kwa silaha za jadi huku akikatwakatwa mapanga na kufanikiwa kuporwa fedha tasilimu.
Taarifa za tukio hilo zinadai kuwa maharamia hao walifanikiwa kupora shilingi milioni 4,500,000.

Licha ya kujeruhiwa mfanyabiashara huyo kadhalika wenzake aliokuwa nao ambao ni Nurudin Mshamu, maarufu kwa jina Chinga(30) aliyekuwa naye akipelekwa kununua mpunga katika kijiji cha Mpanji wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Saturday, November 24, 2012

VIONGOZI WA MAZIWA MAKUU WAJADILI DRC

 
Mkimbizi wa Goma akiingia kambi ya Umoja wa Mataifa nje ya Goma

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa awali juma hili iliishutumu Rwanda kuwa inawasaidia wapiganaji hao, shutuma ambazo zinakanushwa na serikali ya Rwanda.

Kiongozi wa kiraia wa kundi la wapiganaji wa M23 piya yuko kwenye mkutano wa Kampala.

Haijulikani mchango wake ni wa kiasi gani kwenye mkutano huo wa dharura wa viongozi wa kanda ya Maziwa Makuu.

Wapiganaji wanataka kuzungumza ana kwa ana na serikali ya Congo.

Lakini Rais Joseph Kabila anasema atazungumza tu na Rwanda.
Huku nyuma wapiganaji wanaendelea kusonga mbele wakielekea kusini na kaskazini kutoka shina lao mjini Goma.

Umoja wa Mataifa unasema kikosi chake kilioko huko kitajaribu kuwazuwia wapiganaji wasisonge mbele, lakini umesema askari wake wa kuweka amani hawawezi kubeba jukumu la jeshi la serikali ya Congo.(BBC News)

SERIKALI YAOMBWA KUJENGA SOKO LA MAZAO TUNDURU


Na Steven Augustino,
Tunduru.

WAKULIMA  wa zao la korosho wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma wameiomba serikali  kuchukua hatua za haraka, kutatua kero ya kukosekana kwa soko la mazao wanayozalisha hali inayowafanya, kuuza mazao hayo kwa walanguzi wanaotumia kipimo
maarufu kwa jina la Kangomba, ili waweze kusukuma maisha yao ya kila siku.

Pamoja na malalamiko hayo wakulima hao walitumia nafasi hiyo kuishauri halmashauri ya Tunduru kupunguza ushuru wa mazao ambao umekuwa ukitozwa sasa kwa wakulima wake shilingi 200 kwa debe.

Kilio hicho kilipazwa na wakulima hao kupitia mdahalo wa mchakato wakukusanya maoni ya wananchi katika utekelezaji wa shughuli za sekta ya kilimo uliowahusisha wadau wa kilimo kutoka katika  Jimbo la Tunduru Kusini na kufanyika katika  ukumbi wa Skyway mjini hapa.

Friday, November 23, 2012

RAIS ATAKA JINA LA NCHI LIBADILISHWE

Rais wa Mexico amewasilisha mswada kwa bunge la Congress kutaka jina rasmi la nchi hiyo kubadilishwa.

Jina la sasa la jimbo la Mexico lilianza kutumiwa mwaka 1924 baada ya kupata uhuru kutoka Uhispania .

Hata hivyo halijakuwa likitumiwa na rais Felipe Calderon anataka libadilishwe na kuwa Mexico tu.

MZOZO KUHUSU BAJETI YA EU

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamesema kuwa wana shaka ikiwa makubaliano yaliyofikiwa kuhusu bajeti ijayo ya muungano wa ulaya katika mkutano wa EU unaoendelea.

Rais wa ufaransa Francois Holland na Chancella wa Ujeruamani, Angela Merkel walisema hayo baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano huo ambao ulifanyika saa tatu baada ya muda uliotarajiwa kutokana na tofauti zilizokuwepo kuhusu mipango ya bajeti.

MKUU WA MAJESHI DRC AFUTWA KAZI

Generali Amisi.
Mkuu wa majeshi  Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.

Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki.

RAIA KUANDAMANA LEO MISRI

Wafuasi wa Rais wa Misri, Mohamed Morsi, wamesisitiza kuwa madaraka makubwa ambayo amejipatia ni ya muda.

Msemaji wa chama chake cha Freedom and Justice ameiambia BBC, kuwa Bwana Morsi amejipatia mamlaka hayo kwa minajili ya kulinda malengo ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani mtangulizi wake Hosni Mubarak.

Makundi ya upinzani nchini Misri, yameitisha maandamanao ya umma hii leo kupinga uamuzi wa rais wa nchi hiyo wa kujiongezea mamlaka kupindukia.

Kadhalika mmoja wa viongozi wa upinzani, Mohamed El Baradei, amemlaumu Moursi kwa kujiteua mwenyewe kuwa Pharao mpya.

Mamlaka hayo yanampa uwezo rais ambapo maamuzi yake hayawezi kubatilishwa na mamlaka yoyote na hata Mahakama kuu zaidi nchini humo.(BBC News)

CWT YALALAMIKIA UCHELEWESHAJI WA MALIPO YA WANACHAMA WAKE






 Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Gratian Mukoba.(Picha IPP MEDIA)






Na Steven Augustino,
Tunduru.

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, kimelalamikia ucheleweshaji wa malipo ya wanachama wake na kudai kuwa hali hiyo inawafanya wanachama hao kuishi katika maisha ya kuwa omba omba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo jumla ya shilingi 120,423,080 zinazo daiwa na walimu 111  wa wilaya hiyo, yakiwa ni mapunjo yao ya mishahara yaliyolimbikizwa kuanzia mwaka 2009.

Katibu wa chama hicho Bw. Lazaro Saulo alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika ofisini za CWT wilayani humo, na kuongeza kuwa kutokana na hali hiyo pia walimu wengi katika maeneo mbalimbali hivi sasa wanakabiliwa na madeni makubwa ambayo wamekuwa wakikopa kutoka katika asasi za fedha ili kujikimu kimaisha.

MADEREVA PIKIPIKI TUNDURU WALISHUTUMU JESHI LA POLISI


















Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma, Bw. Deusdedith Nsemeki.


Na Steven Augustino,
Tunduru.

Madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la Boda boda wameaswa kuunganisha nguvu zao na kuisaidia serikali kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kudumisha amani na utulivu.

Pamoja na utekelezaji wa maadhimio hayo pia madereva hao wamehimizwa kuwa na leseni za udereva pamoja na kutumia fursa na asilimali zilizopo katika maeneo yao, ili kujiletea maendeleo.

Mwito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho alipokuwa akizungumza na Madereva hao katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Klasta mjini hapa, na kuongeza kuwa endapo wataendelea kujitenga hawatapata mafanikio huku wakihatarisha hali ya amani ya taifa lao, kwani taarifa zao pia zitasaidia kulinda maisha yao na jamii nyingine kwa ujumla.

Akifafanua taarifa hiyo Bw. Nalicho alisema kuwa ili wapate mafanikio kupitia kazi wanazozifanya wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kuwataja wahalifu, ambao ni kati ya wateja ambao kwa namna moja au nyingine huwasafirisha na kuwapeleka katika maeneo ya uhalifu huku wakiwa
wanafahamu au la.

WAKAZI TUNDURU MJINI AFYA ZAO ZIPO HATARINI, WANANCHI WAULALAMIKIA UONGOZI WA WILAYA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu.
















Na Steven Augustino, 
Tunduru.

ABIRIA na Wananchi wanaotumia Kituo kikuu cha mabasi  mjini Tunduru mkoani Ruvuma, wamelalamikia kuendelea kukithiri kwa uchafu katika kituo hicho na kuhofia usalama wa afya zao.

Waandishi wa habari ambao wamezungumza na abiria na baadhi ya wananchi kwa nyakati tofauti, kwa masharti ya kutotajwa majina yao, walisema mbali na kuwepo kwa utaratibu wa halmashauri ya wilaya hiyo, kutoza ushuru wa aina mbalimbali ikiwemo magari yanayoegeshwa katika kituo hicho hali bado ni tete na hakuna juhudi zozote
zinazoonyesha kuzaa matunda katika kukabiliana na suala hilo.

Walisema ushuru ambao hutozwa ni shilingi 1000 kwa kila gari linaloingia na kutoka katika kituo hicho, na magari  yanayoegeshwa ndani ya kituo hicho hutozwa shilingi 1000 kwa kila gari linalo egeshwa hadi asubuhi.

WATENDAJI WA VITONGOJI KATA YA MBINGA MJINI LAWAMANI

















Aliyesimama katika picha ni Mtendaji wa kata ya Mbinga mjini Bw. George Maliyatabu, kulia kwake ni Diwani wa kata hiyo Bw. Kelvin Mapunda na wajumbe wengine. Bw. Maliyatabu alikuwa akiwashutumu na kuwalalamikia watendaji wa vitongoji vilivyopo katika kata hiyo, kwamba wamekuwa ni tatizo katika kuibua miradi mipya ya maendeleo ya wananchi katika maeneo yao ya kazi. Shutuma hizo alizitoa leo mbele ya kikao cha Baraza la maendeleo la kata(WDC) kilichoketi kwenye ukumbi wa Maktaba mjini hapa, na kuwaamuru watendaji hao ifikapo Novemba 24 mwaka huu majira ya asubuhi, wakutane tena katika ukumbi huo na kuanza kupanga upya taratibu za uibuaji wa miradi ya wananchi wa kata hiyo, ili aweze kuwasilisha katika ngazi husika. Miradi hiyo  itakayoibuliwa ni kwa ajili ya mwaka 2013 / 2014.(Picha na Kassian Nyandindi)

Thursday, November 22, 2012

MAPIGANO YAENDELEA GAZA

Mapigano yameendelea usiku kucha katika eneo la Gaza licha ya fununu kuwa kumewekwa mkataba wa kusitisha mashambulio.


Israel inadaiwa kuendeleza mashambulio hayo katika maeneo kadhaa ya Gaza yaliyosababisha kupoteza kwa nguvu za umeme.

Takriban wapalestina ishirini wameripotiwa kuuawa .

AJALI YA GARI

Wakazi wa jiji wakipita kando ya gari Toyota Canter namba T 612 BHY, lililopinduka baada ya kugongana na gari jingine Toyota Canter namba T 529 AAY (halipo pichani). Ajali hiyo ilitokea eneo la Buguruni Barabara ya Mandela, Dar es Salaam jana. (Source Majira newspaper)

Tuesday, November 20, 2012

CHANZO CHA MTO LUHIRA SONGEA CHAPOTEZA MAJI YAKE

















Mshauri wa mtandao wa maji safi katika mamlaka ya maji safi na taka(SOUWASA) manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Bw. Waiton Nyadzi, akionyesha chanzo cha mto Luhira jinsi gani kinavyozidi kupoteza maji yake kutokana na kile alichosema ni sababu ya mabadiliko ya tabia nchi shughuli za binadamu zisizo rasmi.(Picha na Kassian Nyandindi)

MITAMBO YA KUSUKUMIA MAJI SONGEA

















Hii ni mitambo ambayo imejengwa karibu na chanzo cha maji cha mto Luhira, mitambo hii hutumika katika shughuli ya kusukuma maji pale linapotokea tatizo la upungufu wa maji katika manispaa hiyo kama ilivyo sasa.(Picha na Kassian Nyandindi)

MAABARA YA KUTIBU MAJI SONGEA

















Mshauri wa mtandao wa maji safi kutoka mamlaka ya maji safi na taka manispaa ya Songea(SOUWASA) Bw. Waiton Nyadzi, akionyesha waandishi wa habari mitambo inayotumika kuchanganyia dawa ambazo hutumika kuyatibu maji ambayo husambazwa kwa watumiaji katika manispaa hiyo. Maabara ya mitambo hiyo imejengwa katika eneo la Matogoro.(Picha na Kassian Nyandindi)

KUCHUJWA MAJI NA KUYATIBU

















Bw. Waiton Nyadzi ambaye ni mshauri wa maji safi manispaa ya songea katika mamlaka ya maji safi na taka(SOUWASA) aliyenyosha mkono pichani, akiwa katika eneo la mtambo wa kuchuja na kutibu maji akiwapa maelezo waandishi wa habari juu ya maji hayo yanavyochujwa na kuyatibu. katikati ni mwandishi wa habari gazeti la Majira Cresencia Kapinga na kushoto ni Bw. Jaffary Yahaya ambaye ni Mhandisi wa mipango na ujenzi katika mamlaka ya maji safi na taka(SOUWASA) manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.(Picha na Kassian Nyandindi)

MTAALAMU WA MAJI AKIWA NA WAANDISHI WA HABARI RUVUMA

















Mshauri wa mtandao wa maji safi katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kutoka mamlaka ya maji safi na taka(SOUWASA) iliyopo katika manispaa hiyo, aliyenyosha mkono akiwa na waandishi wa habari katika eneo la bwawa kubwa la kuhifadhia maji ambayo yanasambazwa kwa wakazi wa manispaa hiyo kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Bwawa hilo lina urefu meta 83 na upana wa meta 48 huku likiwa na kina cha meta 3.5 lipo katika eneo jirani na milima ya Matogoro(Picha na Kassian Nyandindi)

WAKAZI WA MANISPAA YA SONGEA TUACHE TABIA YA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI




















Kibao hiki ambacho kimewekwa katika chanzo cha maji mto Luhira, kilichopo katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kimewekwa maandishi ya kukataza wananchi wasiweze kuharibu chanzo hicho kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile kilimo. Chakusikitisha baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na chanzo hicho bado wamekuwa ni tatizo ambapo wakati mwingine wamekuwa wakifanya shughuli zisizo rasmi ambazo zimekuwa zikisababisha kupungua kwa maji katika chanzo hicho. Manispaa kwa kushirikiana na wataalamu wake wamekuwa wakitumia nguvu za ziada kudhibiti hali hiyo isiweze kuendelea kuathiri eneo hilo ikiwemo mtu anayekamatwa kuchukuliwa hatua za kisheria kama vile kufikishwa mahakamani. (Picha na Kassian Nyandindi)

KERO YA MAJI SONGEA YAZIDI KUUMIZA VICHWA




















Mshauri wa maji safi katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kutoka mamlaka ya maji safi na taka(SOUWASA) iliyopo katika manispaa hiyo Bw. Waiton Nyadzi, akiwaonyesha waandishi wa habari(Hawapo pichani) ambao walitembelea katika eneo ambalo maji yanachujwa tayari kuingia kwenye bwawa kubwa la kuhifadhia maji lililopo Matogoro katika manispaa hiyo. Waandishi wa habari walifanya ziara leo ya kutembelea eneo hilo kwa lengo la kujua hali halisi ya kero ya upatikanaji wa nishati hiyo muhimu ambayo inalikumba sasa manispaa hiyo.(Picha na nyandindiblog)

Monday, November 19, 2012

KINGA YA ISRAEL DHIDI YA MAKOMBORA

"Iron Dome" ni mojawapo ya kinga nyingi inayomilikiwa na Israel, na inayotumika dhidi ya makombora.

Mfumo huo unatumia rada ili kufuata makombora yanayorushiwa Israel, halafu hufyatua makombora yake ili kuangamiza hayo yanaoyojaribu kupenya.

Mfumo huu ulichukua miaka mingi kujenga na ulianza kutumika mapema 2011.

MAELFU YA RAIA DRC WAWATOROKA WAASI

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo wanasema kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuzorota, huku makumi ya maelfu ya wananchi wakizidi kuwatoroka waasi.

Waasi wa M23 sasa wako kilomita chache tu kutoka mji mkuu wa mkoa wa Goma, hata baada ya kushambuliwa kwa helikopta za Umoja wa Mataifa.

Waasi hao wanasema kwamba hawakusudii kuuteka mji huo, lakini wakazi wanahofia kwamba mji huo utatekwa wakati wowote.

RAIS OBAMA AAHIDI KUISAIDIA BURMA

Obama akiwa ziarani Burma













   
Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kuendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za kuleta mabadiliko nchini Burma.


Katika ziara yake fupi ya kihistoria, Obama alikutana na Rais Thein Sein na kusema uamuzi wa mwisho kuhusu kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Burma kutategemea jinsi taifa hilo litakavyoshughulikia malalamishi yaliyokuwa yametolewa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.

BENKI YA DUNIA YAONYA KUHUSU HALI YA HEWA

Benki ya Dunia imeonya kwamba vipimo vya joto duniani vinaweza kuongezeka kwa alama 4 Celsius ifikapo mwisho wa karne hii, iwapo juhudi zaidi za kutunza mazingira ili kupunguza makali ya kubadilika kwa hali ya hewa hazitachukuliwa.

Ripoti ya benki hiyo imesema kuwa dunia nzima inakumbwa na kupanda kwa viwango vya bahari, ukosefu wa chakula, hali mbaya ya hewa – huku nchi maskini zikiathirika zaidi.

Sunday, November 18, 2012

BALOZI KAGASHEKI ALIA NA WAWINDAJI HARAMU TUNDURU

Bunduki zilizokamatwa katika Oparesheni ya kukamata wawindaji haramu wilayani Tunduru.(Picha na Steven Augustino)


Na Steven Augustino,


Tunduru.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki ameadhimia
kupeleka Bungeni juu ya kubadilisha sheria na kuongeza adhabu
kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai za uhujumu uchumi ambavyo vimekuwa vikifanywa na wawindaji haramu.

Hali hiyo imefuatia serikali baada ya kubaini kushamiri kwa vitendo vya uhalifu na ujangiri, kufuatia oparesheni maalumu iliyofanyika wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, na kufanikiwa kukamata mali zenye thamani ya shilingi milioni 618.408.

Waziri Kagasheki alisema kuwa kuanzia sasa
serikali haitawavumilia na kuwaacha wajanja wachache wakiendelea
kujinufaisha kupitia maliasili za taifa hili, na kwamba alisema adhabu za watuhumiwa hao ni vyema ziwe kati ya miaka 40 na 50.

Aidha pamoja na kuwapongeza askari waliofanikisha kukamata kwa mali hizo Waziri Kagasheki alisema kuwa oparesheni hiyo ni endelevu na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa wilaya hiyo na maeneo mengine kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu, utakaofanikisha kukamatwa kwa wahusika wengine waliokimbia.

MAMA, TUWASALIMIE NDUGU ZETU





Maharusi Joshua na mkewe Frola wakiwasalimia wageni waalikwa katika ukumbi wa familia takatifu Bombambili mjini Songea, baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa la TAG Mjini hapa.(Picha na Muhidin Amri)

SOGEA NIKUPIGE BUSU MAMA!!!

Wakipigana mabusu katika kusherehekea sherehe yao.(Picha na Muhidin Amri)

NJOO NIKUBEBE MAMA, TUFURAHIE NDOA YETU!!!

Bw. harusi Joshua Mwasangapole akiwa amembeba mkewe Frola.(Picha na Muhidin Amri)

TUFURAHIE NDOA YETU MAANA LEO NI SIKU YA PEKEE..........











Maharusi wakiwa katika pozi tofauti, wakifurahia siku yao ya pekee waliyojaliwa na Mwenyezi Mungu katika kufunga pingu zao za maisha.(Picha na Muhidin Amri)

NI FURAHA ILIYOJE LEO KAKA ANAFUNGA PINGU ZA MAISHA




Mdogo wa Joshua  akiimba wakati wa ibada ya ndoa ya kaka yake, katika kanisa la TAG Misufini Songea mjini.(Picha na Muhidin Amri)

BIBI HARUSI NAYE AKUBALI MAPIGO YA NDOA




Bibi Harusi Frola Mwasangapole naye akisaini hati ya ndoa.(Picha na Muhidin Amri)

BWANA HARUSI AKISAINI HATI YA NDOA




Bw. harusi Joshua Mwasangapole akisaini hati ya ndoa baada ya kufunga ndoa katika kanisa ilo, huku mkewe akishuhudia. (Picha na Muhidin Amri)

WAKIFURAHIA TENDO LA KUVESHANA PETE


Bwana harusi Joshua Mwasangapole akimvalisha pete mkewe Frola Mwasangapole wakati wa ndoa yao katika kanisa la TAG Misufini mjini Songea, mkoani Ruvuma  jana.(Picha na Muhidin Amri)

MASHINE HII ITENGENEZWE ILI IWEZE KURAHISISHA KAZI YA KUFUA NGUO





Mkurugenzi wa Veta nyanda za juu Bi. Monica Mbele, akiangali mashine ya kufulia nguo katika hospitali ya misheni Peramiho, ambayo kwa sasa imeharibika.(Picha na Muhidin Amri)

MKURUGENZI WA VETA AKIPOKEA MAELEZO JUU YA DARUBINI INAVYOFANYA KAZI


Mkurugenzi wa Veta nyanda za juu Bi. Monica Mbele akiangalia darubuni katika karakana ya vifaa tiba, Hospitali ya St. Joseph  Peramiho, wengine ni fundi mkuu wa karakana hiyo Bw. Baraka Chumbwi upande wa kushoto na katikati kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Benedict Ngaiza.(Picha na Muhidin Amri)

FUNDI MKUU WA KARAKANA YA PERAMIHO AKITOA UJUZI WAKE

 Fundi mkuu wa karakana ya vifaa tiba katika hospitali ya St. Joseph Peramiho Bw. Baraka Chumbwi akionesha mojawapo ya mashine ya kupiga picha kwa wataalam na mafundi kutoka chuo cha Veta Songea, mafundi kutoka hospitali ya mkoa Ruvuma na ujumbe wa mamlaka ya elimu na mafunzo (VETA) nyanda za juu ukiongozwa na mkurugenzi wake Bi. Monica Mbele.(Picha na Muhidin Amri)

VIONGOZI WAKIPATA MAELEZO JUU YA KITI KINACHOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UPASUAJI


Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma(HOMSO)) Dkt. Benedict Ngaiza upande wa kulia akiwa na mkurugenzi wa Veta nyanda za juu Bi. Monica Mbele wa pili kulia, wakiangalia kiti kinachotumika kwa ajili ya shughuli za upasuaji katika hospitali ya St. Joseph Peramiho. (Picha na Muhidin Amri)

Saturday, November 17, 2012

KIONGOZI AKIPOKEA MAELEZO




Mkurugenzi wa mamlaka ya elimu na mafunzo(VETA) nyanda za juu Bi. Monica Mbele kulia, akimsikiliza fundi mkuu wa karakana ya vifaa tiba katika hospitali ya St. Joseph Peramiho, Bw. Baraka Chimbwi.(Picha na Muhidin Amri)

KIONGOZI AKIWA KATIKA ZIARA

Mkurugenzi wa mamlaka ya elimu na mafunzo(VETA) nyanda za juu Bi. Monica Mbelle akiangalia moja ya vifaa tiba vilivyoharibika katika karakana ya hospitali ya St. Joseph Peramiho Songea vijijini, veta ina tarajia kufundisha wataalam na mafundi wa hospitali mbalimbali kutengeneza vifaa vilivyoharibika ambapo itasaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa kuagiza au kuleta mafundi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya ukarabati wa vifaa hivyo.(Picha na Muhidin Amri)

Wednesday, November 14, 2012

VIONGOZI WAPYA KUCHAGULIWA CHINA

Chama cha Kikomunisti nchini Uchina, kinakamilisha kongamano lake, siku moja kabla ya kutaja viongozi wapya watakaoongoza nchi hiyo kwa miaka Kumi ijayo.

Mwandishi wa BBC, mjini Beijing anasema mkutano huo una mipangilio mahususi kuhakikisha hakuna lolote linaloharibika.

Hatua ya kwanza ni kwa wajumbe zaidi ya elfu mbili kuchagua kamati kuu, ambapo wanachama watakaokiongoza chama hicho, watachaguliwa.

MPAKA WA UGANDA NA DRC KUFUNGWA

Waasi wa M23














Serikali ya Uganda imetangaza kufunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kivuko cha Bunagana.

Hatua hiyo ya serikali ya Uganda inajiri baada ya ripoti moja ya Umoja wa Mataifa kuishutumu Uganda kwa kuwaunga mkono waasi wa M-23 wanaopigana na serikali katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

WANAJESHI KUTUMWA BARAGOI

Polisi aliyejeruhiwa Baragoi














Rais Mwai Kibaki wa Kenya ameidhinisha mpango wa kuwatuma wanajeshi, katika eneo la Samburu Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo kufuatia kuuawa kwa maafisa wa polisi na wezi wa mifugo ambao waliwavizia.

Takriban maafisa 42 wa polisi waliuawa, katika tukio ambalo limetajwa kuwa baya zaidi katika historia ya Kenya.

Baada ya kuongoza kikao cha dharura la baraza la usalama, rais Kibaki amesema, wanajeshi hao wametumwa katika eneo hilo kuwasaka wezi hao wa mifugo na kujaribu kurejesha mifugo hiyo iliyoibwa pamoja na kuwapokonya silaha.

Ripoti zinasema mamia ya watu wametoroka kutoka eneo hilo wakihofia mashambulio ya kulipiza kisasi.

AU KUTUMA WANAJESHI MALI

Waasi wa Mali.













Muungano wa Afrika AU umeunga mkono mpango wa kuwatuma wanajeshi wa kutunza amani nchini Mali, kusaidia katika harakati za kupamabana na wanamgambo wa Kiislamu walioko Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kamati kuu wa muungano huo, imeidhinisha uamuzi uliochukuliwa na Muungano wa Kiuchumi wa nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wa kutuma wanajeshi 3,000 kusaidia serikali ya Mali, kupambana na waasi hao.

Mpango huo sasa utawasilishwa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Wapiganaji wa Kiisalmu na wa kabila la Toureq walichukua udhibiti wa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya rais wa nchi kuondolewa madarakani kufuatia mapinduzi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.

MIGOMO YAANZA ULAYA

Maandamano Ulaya.
















Wafanyakazi katika mataifa kadhaa ya muungano wa Ulaya wameandamana na kufanya migomo kupinga kuongezeka kwa ukosefu wa ajira na mikakati ya serikali ya kupunguza matumizi yake.

Migomo hiyo nchini Uhispania na Uturuki imekwamisha shughuli za usafiri, biashara na shule na maafisa wa polisi wamekabiliana na waandamanaji hao katika mji mkuu wa uhispania Madrid.

Kumekuwepo pia na maandamano katika mataifa ya Ugiriki, Italia na Ubelgiji na maandamano mengine yanatarajiwa katika mataifa mengine.

MWANAJESHI MATATANI - MAREKANI

Waendesha mashtaka wa kijeshi wa Marekani wanataka hukumu ya kifo kutolewa kwa mwanajeshi mmoja anayetuhumiwa kuwaua raia kumi na sita, wakiwemo watoto tisa, Kusini mwa Afghanistan, mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Baadhi ya wanajeshi wamekiambia kikao cha kesi hiyo jinsi Sajenti Robert Bales, alirejea kambini akiwa amelowa damu huku mashahidi wa Afghanistan, wakisimulia alivyofatua risasi kiholela.

Mawakili wa upande wa mshtakiwa hata hivyo wanasema hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mteja wao.

UZOAJI WA TAKA KATIKA MAGHUBA MBINGA UWE ENDELEVU


Katapila la halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, likifanya kazi ya kuchimbua taka katika moja kati ya ghuba la kuhifadhia taka lililopo Mbinga mjini. Uzoaji huo wa taka umeanza kutekelezwa kwa kasi tofauti na hapo awali na hili limetokana na wakazi wa mji huo kulalamika kwa kipindi kirefu kwamba maghuba mengi ya kuhifadhia taka yaliyopo mjini humo, kufurika taka na kukaa muda mrefu bila kuzolewa. (Picha na Kassian Nyandindi).



CHANGAMOTO:

ZOEZI la uzoaji wa taka Mbinga mjini ni jambo la busara ambalo tungependa kuliona linakuwa endelevu.

Jicho letu limeshuhudia changamoto iliyopo sasa ni kwamba wazoaji wanaofanya kazi hiyo wamekuwa wakizoa taka, bila kupewa vifaa kama vile "Gloves" utakuta wanazoa taka bila vifaa hivyo muhimu.

Ni vyema sasa uongozi husika ukachukua jukumu la kuwapa vifaa muhimu ambavyo vitakinga afya zao, zisiweze kushambuliwa na wadudu watokanao na uchafu.

MWAFUTE: UTUNZAJI WA MAZINGIRA NI JUKUMU LETU SOTE

Ofisa misitu wa wilaya ya Mbinga, Bw. Vincent Mwafute.


















Na Mwandishi wetu,
Mbinga.

OFISA misitu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Bw. Vicent Mwafute amewataka wananchi wilayani humo, kuacha tabia ya kukata na kuchoma moto misitu ovyo badala yake waitunze, ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kauli ya ofisa huyo ilifuatia kutokana na kasi ya vitendo vya uchomaji moto misitu inayoendelea kufanyika wilayani humo.

Bw. Mwafute alisema idara yake imekuwa ikitoa elimu mara kwa mara kwa wananchi, juu ya utunzaji wa mazingira lakini watu wachache ndio wamekuwa kikwazo katika kufikia malengo.

Alisema ushirikiano wa dhati unapaswa kuwepo baina ya viongozi, maofisa misitu wa kata na wananchi kwa ujumla katika kukabiliana na suala hili linaloonekana kujitokeza kila mwaka hasa miezi ya Julai, Agosti, Septemba na Oktoba.

Tuesday, November 13, 2012

UPORAJI MKUBWA WA ALMASI ZIMBABWE

 Mgodi wa Marange.













   
Almasi zenye thamani ya dola bilioni 1.25 zimeibwa nchini Zimbabwe. 
Kulingana na shirika la Partnership Africa Canada (PAC), Shirika hilo linasema kuwa huu ndio wizi wa hali ya juu wa Almasi kuwahi kufanywa tangu enzi ya Muingereza Cecil Rhodes aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri wa Almasi.
Shirika hilo linadai kuwa wizi huo uliofanywa katika mgodi wa Almasi wa Marange, uliwanufaisha maafisa wa Zimbabwe, wafanyakazi wa kimataifa wa madini na makundi ya wahalifu.

Afisa mmoja katika sekta ya madini nchini humo, alipuuza madai hayo akasema kuwa ni uongo mtupu.

Ripoti ya shirika hilo ijulikanayo kama, "Reap What You Sow'' ufisadi na uporaji katika mgodi wa Marange, ilitolewa na shirika hilo la nchini Canada, ikinuiwa kwenda sambamba na mkutano wa serikali kuhusu biashara ya Almasi.

Ukiukwaji mkubwa wa sheria:

Rais Robert Mugabe, katika hotuba yake kwa wajumbe alisema kuwa serikali itazingatia sana sheria za kimataifa kuhusu uchimbaji wa Almasi , uhifadhi na uuzaji wake.


Almasi huishia kutengeza pete kama hizi ingawa wanaochimba wanaishi kwa umaskini mkubwa.

Shirika la kimataifa la kuchunguza biashara ya Almasi, (Kimberley Process,) iliondoa marufuku dhidi ya biashara hiyo iliyokuwa imewekewa Zimbabwe mwaka 2011 baada ya kuungwa mkono na Marekani pamoja na Muungano wa Ulaya.

Marufuku hiyo iliwekwa mwaka 2009, kufuatia mauaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu katika mgodi wa Almasi wa Marange pamoja na ripoti kuwa maafisa wa kijeshi walikuwa wanajinufaisha na biashara haramu.

Shirika la PAC lilisema kuwa ukiukwaji huo ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kutisha.

''Tunakadiria kuwa almasi za thamani ya dola bilioni mbili ziliibwa tangu mwaka 2008'', shirika hilo liliongeza.

Mwezi Julai waziri wa fedha wa Zimbabwe Tendai Biti alisema kuwa nchi hiyo inatarajiwa kupata dola milioni 600 kama mapato ya kigeni kutokana na mauzo ya Almasi nje ya nchi, lakini waliweza kupata tu milioni arobaini na sita.(BBC News)

KASHFA YA KAMANDA WA MAJESHI MAREKANI

Kamanda John Allen.













 
Idara ya ulinzi ya Marekani inamchunguza kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, Generali John Allen, kwa kutuma ujumbe usiostahiki wa barua pepe kwa mwanamke aliye na uhusiano na aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, David Petraeus.

Waziri wa usalama Leon Panetta anasema kuwa FBI iliwasilisha kashfa hiyo kwa wizara ya usalama siku ya Jumapili.

AKAMATWA NA SEHEMU ZA SIRI ZA MPWA WAKE

 Ramani ya Afrika kusini.














Mwanaume mmoja nchini Afrika Kusini, amekamatwa baada ya kupatikana akiwa na sehemu za siri kwenye pochi lake ambazo zinaaminika kuwa za mpwa wake ambaye hajulikani aliko.

Msemaji wa polisi, aliambia BBC kuwa baada ya kukamatwa kwake, mwanaume huyo aliwapeleka maafisa wa polisi kwenye msitu katika mkoa wa Eastern Cape, ambako mwili uliokatwakatwa ulipatikana.
Kichwa cha msichana huyo pamoja na miguu yake ilikuwa imekatwa na zilipatikana karibu na kiwiliwili chake.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 42, anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.

Mwanaume huyo alishtakiwa baada ya kushukiwa kuhusika na kutoweka kwa msichana huyo mwenye umri wa miaka 18, aliyepotoea katika mji wa Ngcobo siku ya Jumapili.

Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela alisema kuwa sehemu hizo za siri, zilipatikana ndani ya pochi lake.

Alisema sababu ya kuuawa kwa msichana huyo haijulikani na kwamba uchunguzi unafanyika.

Alipoulizwa ikiwa mauaji hayo yanahusishwa na waganga ambapo sehemu za mwili wa watu hutumiwa kwenye madawa yao, bwana Fatyela alisema kuwa hawezi kubaini hilo kwa sasa.

Kumekuwa na visa vingi vya kuuza sehemu za siri za watu katika sehemu nyingi za Afrika kwa sababu sawa na hizo.

PEMBEJEO ZA KILIMO ZIPELEKWE KWA WAKATI

Utafiti wa mbolea ya Minjingu Hyper pamoja na UREA














Na Mwandishi wetu,
Mbinga.

WAKULIMA wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma wameiomba serikali, kuwapelekea mapema pembejeo za kilimo(ruzuku) ili ziweze kutumika kwa wakati ikilinganishwa na misimu iliyopita, pembejeo hizo zilikuwa zikiwafikia kwa kuchelewa.

Wakulima wa kata ya Kihungu walisema kuwa kuchelewa kuwafikia kwa mbolea hizo, kumekuwa kukiwaathiri na kusababisha washindwe kuzalisha mazao mengi na hivyo kupata hasara.

Mkulima Aderick Komba alisema dhamira ya serikali ya kuwapatia mbolea za ruzuku ni nzuri, lakini imekuwa ikikabiliwa na vikwazo vingi katika usambazaji wake jambo ambalo mwisho wa siku humuumiza mkulima.

TUNDURU WATAKIWA KUJIENDELEZA KIELIMU

MKuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu.

    






 







Na Dustan Ndunguru,
Tunduru.

VIJANA wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wametakiwa kutokata tamaa ya maisha badala yake watumie muda wao kujiendeleza kielimu  ikiwemo kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mafanikio wanayohitaji.

Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya hiyo Bw. Chande Nalicho, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chiwana huku akisema, kama kijana atakuwa hajapata nafasi ya kujiendeleza kielimu ajikite katika shughuli za kimaendeleo.

Bw. Nalicho alisema kuwa vijana wengi wamekuwa na tabia ya kukata tama, jambo ambalo sio zuri na kwamba badala yake wanapaswa kubuni njia mbalimbali za kujiletea maendeleo, ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa vikundi vya uzalishaji mali.

“Kutokana na tatizo la ajira lililopo sasa ni muhimu kwa vijana kutumia akili zao wenyewe kutafuta na kubuni njia bora za kufanya, zitakazowasaidia kujipatia mahitaji yao ya kila siku kuliko kusubiri ajira ambazo hawana uhakika nazo, serikali imeweka mazingira mazuri ambayo yatamwezesha kila anayewajibika kwa lolote kufanikisha”, alisema.