Tuesday, March 28, 2017

SONGEA WAMUOMBA WAKALA WA DANGOTE KUANDAA MASHINDANO YA BONANZA MARA KWA MARA

Na Julius Konala,      
Songea.

BAADHI ya wananchi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameuomba uongozi wa Chuo kikuu cha AJUCO Songea kupitia ufadhili wa Wakala wa usambazaji wa Saruji ya Dangote mkoani hapa, kuandaa mashindano ya bonanza mara kwa mara yatakayolenga kutafuta vijana wenye vipaji maalum ambao wataweza kushiriki katika mashindano mbalimbali yanayofanyika hapa nchini.

Wananchi hao walisema hayo mwishoni mwa wiki wakati walipokuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Songea mara baada ya kuvutiwa na bonanza la michezo lijulikanalo kwa jina la, AJUCO Bonanza 2017 ambalo liliandaliwa na uongozi wa chuo hicho kupitia ufadhili wa Wakala wa usambazaji wa Saruji ya Dangote mkoani humo lililofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji mjini hapa huku washindi wa kwanza wakijinyakulia zawadi mbalimbali.

Bonanza hilo lilitanguliwa na michezo mbalimbali ikwemo kupanda milima ya Matogoro, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mpira wa pete, mpira wa miguu pamoja na shindano la kumtafuta Miss and Mr. AJUCO 2017.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUUNDA CHAMA KITAKACHOTETEA MASLAHI YAO

Katibu Mkuu wa CHODAWU, Said Wamba akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Warsha ya tafiti kwa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CHODAWU, Said Wamba.
WITO umetolewa kwa Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kuunda chama chao cha Wafanyakazi ambacho kitaweza kutetea maslahi yao katika kazi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta isiyokuwa rasmi (CHODAWU), Said Wamba alisema hayo alipokuwa akifungua Warsha juu ya tafiti kwa wafanyakazi hao Jijini Dar es Salaam.

MPITIMBI SONGEA WAJITOKEZA KUTAKA KUPIMIWA MASHAMBA YAO

Na Julius Konala,    
Songea.

ZAIDI ya wananchi 40 wakiwemo wakulima wadogo wadogo katika kijiji cha Mpitimbi A wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, wamejitokeza na kutaka kupimiwa maeneo yao ya mashamba kwa lengo la kupata Hati ya hakimiliki ya kimila baada ya kupewa elimu juu ya matumizi bora ya ardhi, ambayo ilitolewa na shirika lisilokuwa la serikali MVIWATA lililopo mkoani hapa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Michael Ponera alisema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu kijijini humo, akielezea juu ya mwitikio wa wananchi wake namna walivyojitokeza na kuupokea mpango huo mara baada ya kupata elimu hiyo.

Ponera alisema kuwa wananchi hao tangu wapate elimu hiyo juu ya kuweza kutambua masuala ya sheria na umuhimu wa upimaji ardhi sasa wamekuwa wakijitokeza na kujiorodhesha majina yao katika ofisi ya kijiji hicho, wakitaka wapimiwe maeneo yao na kwamba watakapofikia 200 zoezi hilo la upimaji litaanza kwa kuwashirikisha wataalamu wa ardhi kutoka halmashauri ya wilaya ya Songea iliyopo mkoani humo kwa ajili ya kuweza kuwapimia mashamba yao.

Sunday, March 26, 2017

ORODHA YA MAJINA 155 YA MAKATIBU WA CCM WILAYA YA TANZANIA BARA HII HAPA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uteuzi wa watendaji wake katika nafasi ya Makatibu wa Mikoa na Wilaya za Tanzania Bara.









MAKATIBU WAPYA WA CCM MIKOA WALIOTEULIWA HAWA HAPA

1. Arusha - Elias Mpanda
2. Dar es salaam- Saad Kusilawe
3. Dodoma - Jamila Yusuf
4. Geita - Adam Ngalawa
5. Iringa - Christopher Magala
6. Kagera- Rahel Degeleke
7. Katavi- Kajoro Vyahoroka
8. Kigoma- Naomi Kapambala
9. Kilimanjaro- Jonathan Mabihya
10. Lindi-Mwanamasoud Pazi
11. Manyara -Paza Mwamlima
12. Mara -Innocent Nanzabar
13. Mbeya -Wilson Nkhambaku
14. Morogoro- Kulwa Milonge
15. Mtwara -Zacharia Mwansasu
16. Mwanza- Raymond Mwangala
17. Njombe- Hossea Mpagike
18. Pwani- Anastanzia Amasi
19. Rukwa- Loth Ole Nesere
20. Ruvuma- Amina Imbo
21. Shinyanga -Haula Kachambwa
22. Simiyu- Donald Etamya
23. Singida- Jimson Mhagama
24. Tabora- Janeth Kayanda
25. Tanga- Allan Kingazi

JESHI LA POLISI LATHIBITISHA KUKAMATWA KWA MSANII NAY WA MITEGO

Nay wa Mitego.
KAMISHNA msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei ametoa sababu za kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego kwamba kunatokana na kutoa wimbo ambao amedai kuwa unaikashfu serikali ya awamu ya tano iliyopo madarakani.

Matei alifafanua kuwa wimbo huo ambao unaikashfu serikali hiyo unafahamika kwa jina la ‘Wapo’.

Alisema kuwa msanii huyo alikamatwa usiku wa kuamkia leo mkoani humo na kwamba shauri la Nay wa Mitego lipo Jijini Dar es Salaam, hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa huko kwa ajili ya kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo.

Hata hivyo msanii huyo ambaye anafahamika kwa kutoa ngoma zenye ukakasi kwa baadhi ya watu amekamatwa leo akiwa mkoani humo, alipokuwa amekwenda kufanya show.



SAMANDITO: UPIMAJI ARDHI MBINGA UTALETA MANUFAA MAKUBWA KWA WANANCHI

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Gombo Samandito alipokuwa akizungumza hivi karibuni na wakazi wa tarafa ya Mbuji wilayani humo kuhusiana na mpango wa halmashauri hiyo, kuanza mchakato wa upimaji ardhi na kuanzishwa kwa miji midogo sambamba na uendelezaji wa miji hiyo ambapo baadhi ya maeneo yatachukuliwa na serikali kwa ajili ya kupisha huduma mbalimbali za kijamii kama vile ujenzi wa shule, zahanati, miundo mbinu ya maji na barabara.
Wataalamu wa masuala ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, wakiendelea na zoezi la utengenezaji wa Hati za hakimiliki za kimila kwa ajili ya kuwakabidhi wananchi ambao wamepimiwa mashamba yao wilayani humo. 
Na Kassian Nyandindi,   

SIKU zote jamii imekuwa ikitambua kwamba ardhi ni rasilimali muhimu katika kujiletea maendeleo kwa kuitumia kuendeshea shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, ujenzi wa makazi, ufugaji na shughuli nyingine ambapo kutokana na umuhimu wake baadhi ya viongozi kwenye vitongoji na vijiji wamekuwa wakitumia umuhimu wa mahitaji ya ardhi kujinufaisha kwa kuigawa bila kuzingatia sheria, sera na kanuni zilizopo za ugawaji ardhi.

Kutokana na uwepo wa hali hiyo, sasa imekuwa ikisababisha hata kuibuka kwa migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo hapa nchini na haya yote yanasababishwa na viongozi hao kutaka kuingia madarakani kwa kujinufaisha matumbo yao.

Miaka ya 1990 serikali ya Tanzania ilijihusisha katika mchakato wa kutengeneza sera na mfumo wa sheria ambayo ilipelekea uundaji wa sera ya Taifa ya ardhi ya mwaka 1995 na kutungwa kwa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 ambazo ni sheria ya ardhi ya vijiji namba tano ya mwaka 1999 na sheria ya ardhi namba nne ya mwaka 1999 ambapo hizo zote, zimekuwa zikieleza mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji lakini licha ya kuwepo kwa sheria hizo bado changamoto ya migogoro ya ardhi imekuwa ikiendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo.

Aidha juhudi hizo  bado zinahitajika katika kukuza uelewa wa wanakijiji juu ya mifumo ya kisheria katika masuala ya haki za ardhi, uwezo wa uwekezaji mkubwa wa kilimo na uhusiano na ustawi wa wakulima wadogo, kilimo endelevu na maendeleo endelevu ya nchi kwa ujumla.

Hivyo katika kuliona hilo kuwa na umuhimu huo wa kipekee, Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imeweza kuwaelimisha wananchi wake wilayani humo juu ya masuala ya upimaji wa ardhi yao ikiwemo viwanja, mashamba na miji midogo ili kuweza kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima. 
Gombo Samandito akiwa ameshika moja kati ya Hati ya hakimiliki ya kimila.

Migogoro hiyo ya ardhi mingi imekuwa ikijitokeza baina ya wakulima na wafugaji, wakulima na wawekezaji, mtu kwa mtu na kijiji kwa kijiji ambayo wakati mwingine imekuwa ikisababisha watu kupoteza maisha, kupata ulemavu na upotevu wa hata mali zao.

Wengi tumekuwa tukishuhudia kwamba kushamiri kwa migogoro hiyo imekuwa pia ikisababisha kudumaa kwa uchumi wa wananchi kwani wakati mwingine wakulima wamekuwa wakishindwa kuzalisha mazao, wafugaji mifugo yao kujeruhiwa, wawekezaji nao mali zao kuharibiwa na wananchi kutokana na kugombea ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo, makazi na ufugaji.

Mwandishi wa Makala haya amefanya mahojiano na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga, Gombo Samandito ambaye ameeleza kwamba hadi kufikia sasa mashamba yenye zaidi ya ukubwa wa ekari 78,149.065 sawa na hekta 31,259.626 yameingizwa na kupimwa katika mpango wa upimaji ardhi wa wilaya hiyo.

Saturday, March 25, 2017

MAKAMANDA WA POLISI HAPA NCHINI KUPANGA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UHALIFU DODOMA

Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba.
Na Frank Geofray - Jeshi la Polisi.

MAOFISA Wakuu wa Polisi  wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu Machi 27 hadi 29 mwaka huu, katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao makuu ya Polisi, makamanda wa Polisi wa mikoa na Makamanda wa vikosi vya bara na Zanzibar ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji kazi kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka huu 2017.

POLISI WAMSAKA ALIYEMTOLEA NAPE BASTOLA

JESHI la Polisi limesema kwamba limeanza kufanyia kazi maagizo waliyopatiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kumsaka mtu aliyemtolea bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Hayo yalisemwa jana na Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso ambapo awali, alipotafutwa Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu, lakini simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyemtaka mwandishi amtafute Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ili atoe ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa agizo la Waziri Nchemba.

Alipopigiwa simu, Senso alijibu kwa ufupi kuwa wameanza kufanyia kazi agizo la Waziri Nchemba.

MHANDISI IDARA YA UJENZI MBINGA ATUMBULIWA KWA MAKOSA YA UZEMBE NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA

Na Kassian Nyandindi,       
Mbinga.

HALMASHAURI ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imechukua hatua ya kumsimamisha kazi Kaimu Mhandisi wa idara ya ujenzi wilayani  humo, Anyitike Kasongo kutokana na kubainika kufanya makosa ya uzembe na ubadhirifu wa mali za umm

Anyitike Kasongo.
Aidha imeelezwa kwamba kusimamishwa huko ambako ni kwa muda usiojulikana kunalenga kupisha uchunguzi na baadaye atachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria na taratibu husika.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga, Gombo Samandito alisema hayo alipokuwa akizungumza juzi na waandishi wa habari ofisini kwake.

Samandito alisema kuwa sababu ya kusimamishwa huko anadaiwa kufanya ubadhirifu na wizi wa mali za umma katika kazi ya ujenzi wa kibanda cha mlinzi chenye thamani ya shilingi milioni 19,000,000 kwenye nyumba ya kuishi Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Mbinga ambayo imejengwa mtaa wa Kipika mjini hapa.

SISTA KANISA KATOLIKI MBINGA AFIKISHWA MAHAKAMANI AKIDAIWA KUIBA MAMILIONI YA FEDHA ZA KANISA

Na Kassian Nyandindi,    
Mbinga.

KANISA Katoliki Jimbo la Mbinga wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, limemfikisha Mahakamani Sista mmoja wa kanisa hilo ambaye anafahamika kwa jina la Emmanuela Nindi (40) kwa tuhuma ya kuliibia kanisa shilingi milioni 28.8 ambazo ni mali ya jimbo hilo.

Sista huyo ambaye alikuwa ni Mhasibu wa jimbo hilo, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo kwa lengo la kumtaka ajibu shtaka hilo linalomkabili mbele yake.

Ilidaiwa na Mwendesha mashtaka wa Polisi Inspekta, Seif Kilugwe mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mbinga, Magdalena Ntandu kwamba mshtakiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo katika kipindi cha mwaka jana.

Friday, March 24, 2017

WASHIRIKI WA MAFUNZO JUU YA MATUMIZI BORA YA ARDHI SONGEA WALALAMIKIA KUKOSA USHIRIKIANO TOKA OFISI ZA VIJIJI

Na Julius Konala,   
Songea.

MTANDAO wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mkoani Ruvuma, kupitia ufadhili wa shirika la Tanzania Foundation for Civil Society (FCS) umeendesha mafunzo juu ya matumizi bora ya ardhi kwa wakulima wadogo wadogo wanaotoka katika kata nne wilayani Songea mkoani humo.

Mafunzo hayo yalifanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha ushirika kilichopo katika Manispaa ya Songea ambayo yalifunguliwa na Mwenyekiti wake Asumpta Ndauka, ambapo washiriki hao wametakiwa kuzingatia sheria na taratibu husika za mafunzo hayo waliyopata kwani wao ndio waathirika wakubwa wa migogoro ya ardhi vijijini.

Aidha mafunzo hayo yalishirikisha washiriki 200 wa kutoka katika kata ya Magagura, Mpitimbi, Mpandangindo na Mbingamhalule wilayani humo na kwamba Mwenyekiti huyo amewataka pia wanawake kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki zao juu ya umilikishwaji wa ardhi na kupata hati miliki kwa madai kuwa wao wamekuwa wakikosa fursa hiyo kutokana na uwepo wa tatizo la mfumo dume.

Monday, March 20, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: RAIS DKT. MAGUFULI NA RAIS WA BENKI YA DUNIA DKT. JIM YONG KIM UWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI BARABARA ZA JUU JIJINI DAR ES SALAAM

            Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa makutano ya barabara za juu katika eneo la Ubungo Interchange Jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.
           Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuzindua mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa makutano ya barabara za juu za Ubungo Jijini Dar es Salaam.
           Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo (Ubungo interchange) zitakavyokuwa.
             Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo Jijini Dar es Salaam.
            Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na             Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwapungia wananchi mkono               wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya barabara za juu                                Ubungo interchange, Ubungo Jijini Dar es Salaam.
                    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli                    akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais                  wa benki ya dunia Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati                     wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya                       uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo                                          interchange, Ubungo Jijini Dar es Salaam.
                    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli                      akizungumza jambo na Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati                    wakiwa ndani ya moja ya basi la DART wakati wakitokea kituo kikuu cha                   BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi               wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo Jijini Dar es                                                                  Salaam.
                     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli                     akimkaribisha Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya                                             kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
                 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli                    akizungumza na Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya                  kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
          Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.
                   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli           akiwa na mgeni wake Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiagana na wananchi wa Kivukoni hawapo pichani kabla ya kupanda Basi la Mwendokasi (DART) kuelekea Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi Mradi wa Makutano ya barabara za juu za Ubungo Jijini Dar es Salaam.
                      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli                         akimshukuru Rais wa benki ya dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada                       ya kutoa hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Makutano                        ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo Jijini Dar es Salaam.
                       Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipanda basi la DART-maarufu                           kama Mabasi ya Mwendokasi katika eneo la Kivukoni wakati akielekea                       Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi                    wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo Jijini Da es Salaam.
       Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ndani ya basi la Mwendokasi wakati   akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa     Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo Jijini Dar es Salaam.
                  Baadhi ya Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa                    na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli                kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa makutano ya barabara za              juu Ubungo interchange, Ubungo Jijini Dar es Salaam - Picha zote na Ikulu.

RAIS MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KULINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi leo Jijini Dar es Salaam.
Na Daudi Manongi,  Maelezo.

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Watanzania hapa nchini kuulinda mradi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 188 na kukamilika mwaka 2019. 

Rais Magufuli alisema hayo leo wakati alipokuwa akitoa hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hizo katika eneo la Ubungo Jijini hapa. 

“Tutasimamia fedha hizi kikamilifu ili tuweze kujenga barabara hizi za juu vyema, nawataka Watanzania wenzangu kusimamia mradi huu ipasavyo ili ukamilike haraka na hivyo wizara, mkandarasi na msimamizi wa mradi huu uweze kukamilika na kuleta tija kwa wananchi wetu”, alisisitiza Rais Magufuli. 

NAPE AUNDA KAMATI KUCHUNGUZA TUKIO LA UVAMIZI KITUO CHA HABARI CLOUDS MEDIA

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika Picha) alipofanya ziara katika Chombo cha Habari cha Clouds Media Group leo Jijini Dar es Salaam.
                Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye                       Katikati, akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya                   Habari  Nchini (MOAT) Reginald Mengi (kulia) alipofanya ziara katika chombo cha Habari leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbas.
              Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye                       (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Joseph                 Kusaga (wa pili kushoto) alipowasili katika ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam,             wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Dkt. Hassan Abbas (Pembeni             ya Waziri) na wa kwanza kushoto ni Afisa Mahusiano wa Clouds Simon                                                                       Simalenga.
                  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye                  (katikati) akielezwa jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo                vya    Habari Nchini (MOAT) Reginald Mengi (kulia) alipotembelea Ofisi hizo            leo Jijini          Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media                                                            Joseph Kusaga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye                   (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya                                            Jamii Peter Serukamba (MB).
             Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya jamii wakimsikiliza Mwenyekiti wa              Kamati hiyo (hayupo katika picha) Peter Serukamba (MB) walipotembelea Kituo cha                               Habari cha Clouds leo Jijini Dar es Salaam. 
Na Mwandishi wetu,

WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye ameunda Kamati ya watu watano itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbas kuchunguza tukio la uvamizi lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika chombo cha habari cha Clouds Media.

Akiongea katika ziara aliyoifanya  leo  Jijini Dar es Salaam  katika chombo hicho Nape alisema kuwa Kamati hiyo itafanya kazi ndani ya masaa 24 kuanzia sasa huku akiwataja wajumbe wengine  kuwa ni Frank Balile, Johanes Neng’ida, Jessy Kwayu na Mabel Mabisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Serikalini (TCRA).

“Kamati hii ipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili tuwe na taarifa iliyokamilika na kujua hatua itakayofuata”, alisema Nape.

COPE YAKUSUDIA KUBORESHA MNYORORO WA THAMANI YA MAZIWA SONGEA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge aliyekuwa upande wa kushoto akimsikiliza Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la serikali la COPE kutoka nchini Italia Valentina Quaranta ofisini kwake mjini Songea jana, ambapo shirika hilo linakusudia kuwekeza katika mradi wa kuboresha mnyororo wa thamani ya uzalishaji wa maziwa katika halmashauri tatu za mkoa huo yaani Songea Manispaa, halmashauri ya wilaya ya Songea na Namtumbo.

RC RUVUMA AWATAKA WAKULIMA WA MPUNGA NYASA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge akiangalia kibanio kinachotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa zao la Mpunga katika mto Wabu halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani humo ambapo wakulima hutegemea mto huo kwa ajili ya kuzalisha zao hilo kwa manufaa ya maendeleo yao ambapo Dkt. Mahenge alisisitiza pia kwa kuwataka wakulima hao waitunze miundombinu ya kilimo hicho.

UJENZI WA DARAJA MTO RUHUHU UMESIMAMA KUTOKANA NA KUKOSEKANA VIFAA VYENYE UWEZO WA KUCHIMBA MASHIMO YA KUSIMAMISHA NGUZO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho upande wa kulia akiangalia hivi karibuni Kalavati linalojengwa katika mto Ruhuhu ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa daraja kubwa katika mto huo linalounganisha wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma na wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe, hata hivyo ujenzi wa daraja hilo umesimama kufuatia kukosekana kwa baadhi ya vifaa vyenye uwezo mkubwa wa kuchimba mashimo ya kusimamisha nguzo za daraja hilo litakalojengwa.

TUKIO KATIKA PICHA: WENYEVITI WA MITAA MANISPAA SONGEA WALALAMIKIA WATUMISHI WA MANISPAA HIYO

Mwenyekiti wa mtaa wa Mahenge B katika Manispaa ya Songea Adili Mchome akitoa malalamiko yake na ya Wenyeviti wenzake wa mitaa mbalimbali katika Manispaa hiyo juzi kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge hayupo pichani, juu ya dharau wanayofanyiwa na baadhi ya watumishi wa Manispaa kila wanapokwenda katika ofisi za serikali kwa ajili ya kupata huduma na miongozo mbalimbali itakayoweza kuwasaidia namna ya kuboresha utendaji wa kazi zao za kila siku, kikao hicho kilifanyika mjini hapa ambapo Dtk. Mahenge alikemea hali hiyo na kuwataka watumishi hao wafanye kazi kwa kuheshimu watu na kuzingatia maadili ya kazi zao.