Na Muhidin Amri,
Songea.
IDADI ya watu walioathirika kutokana
na kunywa kinywaji aina ya togwa ambacho kinasadikiwa kuwa na sumu, katika
kijiji cha Litapaswi kata ya Mpitimbi wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,
imeongezeka kutoka 250 na kufikia watu 325.
Akizungumza na Waandishi wa habari mjini
hapa, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Mihayo Msikhela alisema tukio ilo limetokea
juzi katika kijiji hicho, wakati watu hao wakiwa kwenye sherehe ya kipaimara ya
mwanafunzi wa darasa la sita Dickson Nungu ambaye anasoma shule ya msingi Litapwasi.
Kamanda Mihayo alifafanua kuwa kati ya waathirika hao watu 29 wamelazwa katika hospitali ya misheni Peramiho, ambapo kati yao wanaume wapo wane na wanawake 22.
Aidha watoto wapo watatu huku wengine
295 wamefikishwa katika zahanati ya Lyangweni ambao wanaume ni 118,
wanawake 148 na watoto 29.
Katika waathirika hao tayari wengine 225 wameshatibiwa na kuruhusiwa huku watu 71 bado wanaendelea kupatiwa huduma katika kituo cha matibabu kilichopo shule ya msingi Kiwalawala.
Kufuatia tukio hilo watu watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma kuhusiana na tukio hilo, ambapo kwa mujibu wa Kamanda Mihayo aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Ernest Nungu, Benedict Nungu Esebius Komba, Sadik Masoud na John Kaulangudidi wote wakazi wa kijiji cha Litapwasi.
No comments:
Post a Comment