Mzee Asteri Ndunguru, upande wa kulia akisoma taarifa fupi ya marahemu Menas Mbunda Andoya nyumbani kwa marahemu mjini hapa. |
Mwili wa marahemu Menas Mbunda Andoya ukiombewa katika kanisa la Mtakatifu Killian lililopo mjini Mbinga. |
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma naye alishiriki katika ibada ya mazishi hayo, kwenye kanisa la Mtakatifu Killian Mbinga mjini. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
WAKRISTO wametakiwa kuacha matendo ya kumpuuza mwenyezi
Mungu, badala yake wametakiwa kutenda mema katika maisha yao ya kikristo kwani
hakuna binadamu aliyefunga mkataba na Mungu juu ya kuishi.
Hayo yalisemwa na Askofu mkuu wa jimbo la Mbinga mkoani
Ruvuma, John Ndimbo alipokuwa akihutubia katika misa takatifu ya mazishi ya
marahemu Menas Andoya kwenye kanisa la mtakatifu Kiliani lililopo mjini hapa.
“Miili yetu ni hekalu la bwana na maskani ya mpito hapa
duniani, inatupasa kufanya kila jitihada kwa mambo ambayo yanampendeza Mungu,
hakuna binadamu asiyekuwa na utashi juu ya kifo”, alisema Ndimbo.
Alisema Mungu anao uwezo wa kumchukua yule mtu ambaye
binadamu walimtegemea kwa namna moja au nyingine kwa lengo la hapa duniani kwa mambo maovu na kumuweka
sehemu ya milele mahali pema peponi.
Akielezea wasifu wa marahemu huyo, Askofu Ndimbo alisema kuwa
alikuwa ni mtu ambaye tegemeo kubwa kwa wanambinga kupitia huduma zake
alizokuwa akizitoa katika jamii.
Kadhalika marahemu Andoya, alikuwa ni Mkurugenzi wa kampuni ya Andoya
Hydro Electric Power (AHEPO) ambao ni mradi mkubwa wa umeme wa maporomoko ya
maji alioubuni mwaka 2000 na kufanikiwa kuwasha umeme kwa majaribio.
Madhumuni ya kuzalisha umeme katika mradi huo ni Megawati 1
na kuunganishwa kwa wateja wa awali 922 kati ya 3,835 katika vijiji vya
Lifakara, Kilimani na Mbangamao wilayani Mbinga na ziada kuuzwa katika shirika
la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) ukilenga kupata umeme kwa njia endelevu na
nafuu.
Hivi sasa tayari ujenzi wa njia kuu za kusafirisha umeme
kutoka Mbinga mjini, hadi kituo kikuu cha uzalishaji na usambazaji katika
vijiji hivyo umekwisha kamilika.
No comments:
Post a Comment