Na
Steven Augustino,
Tunduru.
BINTI
wa miaka mitano Mwanahamis Omary, mkazi wa kijiji cha Kalulu wilayani Tunduru
mkoa wa Ruvuma, amekutwa akiwa amefariki dunia baada ya kuumwa na nyoka mwenye
sumu kali.
Akizungumzia
tukio hilo baba wa mtoto huyo Omary Bakari alisema mkasa huo ulimpata mtoto
huyo, wakati akiwa anavuka mto Kalulu kuelekea shambani na kwamba wakati
anakumbwa na tatizo hilo alikuwa amefuatana na mama yake mzazi Zainabu Ally.
Baada
ya tukio hilo mama yake huyo alipiga kelele za kuomba msaada wa kumpeleka mtoto
wao katika zahanati ya kijiji hicho kwa matibabu zaidi, lakini ilishindikana
kwani mtoto huyo alifariki dunia wakiwa njiani kuelekea katika zahanati hiyo.
Hata
hivyo nyoka huyo hakuweza kutambuliwa ni wa aina gani, wakati anamuuma mtoto
huyo.
No comments:
Post a Comment