Na
Steven Augustino,
Tunduru.
KIJANA
mwenye umri wa miaka 15 aliyefahamika kwa jina la Khasim Mohammed, mkazi
wa kijiji cha Mtangashari wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma amefariki dunia baada
ya kupata ajali katika gari, ambalo alikuwa ameomba msaada ili aweze kusafiri.
Mihayo
Msikhela kamanda wa polisi wa mkoa huo, alisema kuwa marahemu huyo alifariki
dunia papo hapo baada ya kuanguka katika gari hilo.
Alisema
ajali hiyo ilitokana na gari lenye namba za usajiri T699 BCX mali ya kampuni ya
China Civil Engineering Construction Co.Ltd (CCECC) inayojenga kipande cha barabara
kilometa 58.7 kutoka Tunduru mjini hadi Matemanga.
Alisema
baada kijana huyo kulisimamisha gari hilo dereva wa lori hilo aina ya SEYA 33G
ambalo ni maalum kwa ajili ya kubebea kifusi, alisimama na kufanya makubaliano ya
kumchukua hadi Tunduru mjini.
Alifafanua
kuwa lori hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Fredy Chasua, ambapo ghafla
aliliondoa gari hilo wakati kijana huyo akiwa anaendelea kupanda hali ambayo
ilimfanya ateleze na kuanguka chini, na kukanywagwa na magurudumu ya nyuma na
kusababisha kifo chake papo hapo.
Kamanda
Msikhela aliendelea kufafanua kuwa baada ya tukio hilo, dereva huyo alikimbia
na kutokomea kusiko julikana, na kwamba Polisi wanaendelea kumsaka ili sheria
iweze kufuata mkondo wake.
No comments:
Post a Comment