Na Steven Augustino,
Tunduru.
POLISI
wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, wanamsaka dereva aliyekuwa akiendesha pikipiki
aina ya SUNLG yenye namba za usajiri T 115 CZE ili aweze kujibu mashitaka ya
mauaji aliyoyafanya baada ya kumgonga mwendesha baiskeli.
Dereva
huyo ambaye jina lake halijafahamika anadaiwa kufanya mauaji hayo, Disemba 13
mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi katika kijiji cha Tuleane kilichopo Tarafa
ya Mlingoti – Namasakata mjini hapa.
Imeelezwa
na Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Mihayo Msikhela kuwa mauaji hayo aliyafanya
kwa kumgonga na pikipiki Rashid Tawakali (50) wa kijiji cha Nakayaya wilayani
humo na kumsababishia kifo papo hapo.
Msikhela
alisema baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo ametokomea kusikojulikana, na kuitelekeza
pikipiki hiyo katika eneo la tukio baada ya kumgonga mwendesha baiskeli huyo na
kusababisha kifo chake.
Alisema
baada ya tukio hilo mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti kilichopo katika hospitali ya serikali wilayani Tunduru na baadae ndugu
wakafanikiwa kuutambua mwili wake na kuruhusiwa kwenda kumzika.
Kamanda
Msikhela ametoa wito kwa wananchi wanaojua taarifa zozote juu ya mmiliki au
dereva wa pikipiki hiyo, kuwasaidia ili kuwezesha kumkamata na sheria iweze
kuchukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment