Na Mwandishi wetu,
Tunduru.
STAMILI Mohamed (42) ambaye ni mkazi wa kijiji cha
Namiungo wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, amekutwa na mauti baada ya pikipiki
aliyokuwa akiiendesha kupata nayo ajali, akiwa katika mwendo kasi.
Taarifa zinaeleza kuwa pikipiki hiyo aliyopata nayo
ajali, ni aina ya SUNLG yenye namba za usajili T 339 na kwamba ajali hiyo,
ilitokana pia na kuligonga trekta dogo ambalo hutumika kufanyia shughuli za
kilimo shambani (Power tiller) na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amethibitisha kuwepo kwa tukio
hilo, akieleza kwamba ajali hiyo ilitokea Disemba 4 mwaka huu majira ya usiku.
Awali alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo
kasi aliokuwa nao mwendesha pikipiki huyo, marehemu Mohamed hali ambayo
ilimfanya ashindwe kukwepa Power tiller hilo lililokuwa mbele yake.
Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo,
Dokta Joseph Ng’ombo alisema kuwa kifo hicho kilisababishwa na kuvuja kwa damu
nyingi ndani kwa ndani, kulikosababishwa na marehemu kujigonga katika bodi trekta hilo.
Dokta Ng’ombo alisema katika ajali hiyo marehemu
alipata mivunjiko katika mifupa na mbavu zilizoshikilia kifua, pamoja na
kuvunjika mguu wa kushoto mara mbili hali ambayo ilisababisha kutokwa na damu
nyingi.
No comments:
Post a Comment