Na Kassian
Nyandindi,
Mbinga.
NDUGU
wasomaji wa mtandao huu, sasa tunawaletea taarifa ya Mkaguzi wa ndani
juu ya hoja zilizojitokeza katika
kikao cha fedha, mipango na uongozi kilichoketi Septemba 25 mwaka huu
wilayani
Mbinga mkoa wa Ruvuma, na kuwasilishwa katika kikao cha baraza la
madiwani la
wilaya hiyo Oktoba 27 mwaka huu, kama tulivyosema kuwa katika toleo lililopita kwamba Madiwani walinyang'anywa mara baada ya kusomwa katika
baraza hilo.
Taarifa
hiyo ambayo imesainiwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
hiyo Hussein Ngaga ina hoja saba za kumtuhumu Afisa
elimu wake wa idara ya elimu msingi wilayani humo, Mathias Mkali kwamba amefanya
ukiukwaji
mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu za fedha za utumishi wa umma, jambo
ambalo baadhi ya Madiwani wengi wao walipinga hoja hizo na kusema kuwa jambo hilo halina kweli
badala yake ni mambo ambayo
yalikwisha kubaliwa na kupitishwa kwenye vikao halali na baraza la madiwani kwa ujumla. (nakala tunazo)
Katika
hali ya
kushangaza, taarifa hiyo iligawiwa kwa madiwani katika baraza hilo,
ghafla wajumbe husika (Madiwani) baada ya taarifa hiyo kumaliza kuisoma mkaguzi wake wa ndani, Laston Kilembe na madiwani hao kuipinga, ghafla madiwani walinyang’anywa huku
mkurugenzi akisimama
mbele ya kikao na kueleza kuwa haijakamilika watapatiwa tena katika
kikao
kijacho cha baraza hilo.
Sasa taarifa yenyewe ni hii hapa.............................
No comments:
Post a Comment