Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu. |
Na
Kassian Nyandindi,
MATUKIO
ya mabomu mjini Songea hapa mkoani Ruvuma, umekuwa sasa ni mchezo mchafu ambao
unahatarisha usalama wa raia, hivyo kuna kila sababu kwa serikali kuchukua
hatua madhubuti juu ya kudhibiti hali hii.
Tunasema
kuna kila sababu sasa ya kufanya hivyo, kutokana na kile tunachoweza kusema
kwamba tumechoka kusikia kauli za viongozi wa ngazi ya juu hususani hapa
mkoani, wakisema kwamba watahakikisha hali hii itadhibitiwa kwa kuwakamata
wahusika ili matukio kama haya yasiweze kuendelea kutokea.
Ni
muhimu sasa kuona namna gani tunashirikisha jamii kwa karibu zaidi, ili waweze
kutoa ushirikiano wa kutosha ambao baadaye utaweza kuleta tija katika kukomesha
genge la watu hawa, ambao wanahusika kutengeneza mabomu haya.
Hili
ni tukio la tatu sasa kutokea hapa songea, mara ya kwanza askari polisi
walirushiwa bomu, mara ya pili lilitegwa karibu na kituo cha kurusha matangazo
(TBC) mjini Songea na leo askari hawa hawa wanarushiwa tena, tunapenda kuhoji
vyombo vya ulinzi na usalama vipo wapi au vimeenda likizo?
Tunahoji
hivyo sio kwa nia mbaya, kwa sababu mara kwa mara tumekuwa tukiwanukuu baadhi
ya vigogo wakisisitiza na kuahidi kukomesha hali hii isiweze kuendelea kutokea,
lakini inashangaza kuona matukio haya yanajirudia na kuwafanya watu waishi kwa
wasiwasi.
Leo
Songea imefikia hatua ya kulipuliwa mabomu, yatupasa sasa viongozi husika
tuache kukaa maofisini na kuishia kusoma mafaili tu, twendeni huku na kule
tukachunguze ili tuweze kukomesha hali hii ambayo inahatarisha usalama wa raia
wetu.
Mara
kwa mara timu ya wataalamu wa kuchunguza mambo tumeshuhudia ikiundwa, lakini
hatma ya kazi wanayofanya hatuoni kuzaa matunda ipasavyo ndio maana genge la
wahuni ambao wanamazoea ya kutengeneza mabomu, wamekuwa wakiendelea kutamba na
kujeruhi askari wetu ambao hawana hatia.
Katika
kuyasemea haya nashauri pia ulinzi uimarishwe pande zote za mkoa wetu wa
Ruvuma, hata sehemu zenye mipaka ambayo tumepakana na nchi jirani huenda wahalifu
hawa wakatokea huko na kuja kuleta vurugu hizo, ambazo zina hatarisha ustawi wa
maendeleo katika mkoa wetu na taifa kwa ujumla.
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu wewe ndiye baba yetu na Mwenyekiti wa Kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa huu, ni wakati sasa wa kuhakikisha unapambana
ipasavyo juu ya matukio haya, ambayo yanaharibu na kuchafua sifa ya mkoa wetu.
Tunategemea
siku moja genge hili la wahuni wanaozalisha mabomu na kujeruhi askari wetu,
litafahamika na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo hata kufungwa jela maisha
ili kuwatokomeza kabisaaa………. na wasionekane tena wakiranda randa mitaani na
kuhatarisha usalama wetu.
Nasema
ifike mahali hakuna haja ya kulala usingizi tena, tuchape kazi usiku na mchana
ili tuweze kubaini kiini cha shetani huyu wa mabomu kipo wapi hapa kwetu mkoani
Ruvuma na tukisha baini ukweli ni wapi wapo, hatua zichukuliwe haraka
iwezekanavyo.
Mwenyezi
Mungu ibariki Tanzania na mkoa wetu wa Ruvuma!
Mwandishi
wa makala haya anapatikana kwa barua pepe, nyandindi2006@gmail.com.
No comments:
Post a Comment