Steven Augustino na Abbas Mlanya,
Ruvuma.
WATU
wawili wamefariki dunia mkoani Ruvuma, katika matukio mawili tofauti
yaliyotokea wilayani Tunduru na Namtumbo mkoani humo, ambapo la kwanza linasababishwa
na wivu wa kimapenzi na lingine linahusishwa na mambo ya ushirikina.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio lililotokea wilayani Tunduru, walisema kuwa marahemu aliyetambuliwa
kwa jina la Yusuph Jafari ambaye amehamia wilayani humo, akitokea wilaya ya Masasi
alikuwa kinara wa kutembea na wake za watu na baadaye kuuawa na watu
wasiojulikana.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma, ASP Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio la kwanza
lilitokea Disemba 16 mwaka huu katika kitongoji cha Naunditi kijiji cha Majimaji,
kilichopo kata ya Muhuwesi wilayani humo.
Alisema
katika tukio hilo Yusuph jafari (54) alikutwa akiwa amefariki dunia nje ya
nyumba yake, huku akiwa amekatwakatwa kwa mapanga na mwili wake ukiwa umetelekezwa
nje ya nyumba yake.
Kuhusu
tukio la pili ambalo lilihusishwa na mambo ya kishirikina lililotokea wilayani
Namtumbo, ambapo kamanda Msikhela nalo amethibitisha likimhusisha mzee mwenye
umri wa miaka 64 aliyetambuliwa kwa jina la Yasin Fussi.
Tukio
hilo imeelezwa kuwa lilitokana na wananchi kuchukua sheria mkononi wakimtuhumu kikongwe
huyo, kumpoteza mtoto wake katika mazingira ya kutatanisha kwa njia za
ushirikina.
Msikhela
alifafanua kuwa mzee huyo, aliuawa akituhumiwa kumficha mtoto wake aliyetajwa
kwa jina la Kassim Fussi anayedaiwa kutoweka Disemba 14 mwaka huu.
Alisema
baada ya tukio la kutoweka kwa kijana huyo wananchi walimwita mzee huyo na
kumhoji juu ya tukio hilo, lakini hakutoa maelezo yoyote hali ambayo iliwatia shaka
na hasira iliyosababisha kuchukua maamuzi hayo magumu.
Kufutia
hali hiyo Jeshi la Polisi linawaomba wananchi wenye taarifa juu ya matukio hayo,
kutoa ushirikiano kwa kuwataja wahusika ili waweze kukamatwa na kutoa nafasi
kwa vyombo vya sheria, kuchukua mondo wake.
No comments:
Post a Comment