Rais Jakaya Kikwete, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. |
Na
Kassian Nyandindi,
Mbinga.
SIRI
juu ya mipango ambayo inaendelea kusukwa chini kwa chini, katika kuhakikisha
kwamba Afisa elimu msingi wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Mathias Mkali
anachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa Mahakamani, kufuatia mgogoro
uliotengenezwa na Mkurugenzi wake wa Halmashauri ya wilaya hiyo Hussein Ngaga,
zimeanza kuvuja ambapo mtandao huu umeelezwa.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari vimeeleza na kudai kwamba
licha ya kuwepo kwa mipango ya kufikishwa Mahakamani Afisa elimu huyo, huenda
kama itashindikana katika hilo atachukuliwa hata hatua ya kuhamishwa, ilimradi adhma ya mkurugenzi huyo iweze
kutimia kama alivyopanga.
Serikali
licha ya kuunda tume na kuja kuchunguza tatizo hili linaloendelea sasa kukera
wananchi wa Mbinga, imeonekana tume hiyo kumezwa na vigogo wa halmashauri hiyo wakitaka
ilinde maslahi yao binafsi, ikiwemo hudaiwa kushiriki kwa namna moja au nyingine
katika kupanga mipango hiyo.
Utafiti
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa, kumekuwa na vikao ambavyo
vimekuwa vikifanyika mara kwa mara katika Ikulu ndogo ya Rais wilayani hapa,
kati ya vigogo wa wilaya hiyo na wajumbe husika wa tume hiyo hasa nyakati za
usiku na mapema alfajiri.
Wadau
wa elimu mjini hapa wamekuwa wakihoji, inakuwaje jambo hili la wao kuendelea
kukaa katika Ikulu hiyo na kufanya vikao kwa majira hayo jambo ambalo linatia shaka,
wakidai kuwa huenda kuna mipango michafu ambayo inaendelea kusukwa chini kwa
chini kwa lengo la kulinda maslahi yao binafsi.
Kadhalika
kufuatia hali hiyo, baadhi ya wakazi wa wilaya ya Mbinga wameeleza kuwa ni
vyema serikali ikachukua hatua ya kufanya mabadiliko ya uongozi wilayani humo,
ikiwemo hata kumhamisha mkurugenzi mtendaji au kumchukulia hatua nyingine za kinidhamu ili kuweza kunusuru migogoro ya
hapa na pale isiweze kuendelea, ambayo yeye ndiye kinara wa kuitengeneza na kutishia ustawi wa maendeleo wilayani hapa.
Mkurugenzi
Ngaga anakuza mgogoro huo ambao umejenga hata nyufa na kutengeneza makundi kwa baadhi ya watendaji
wa serikali na madiwani, kufuatia kwa kile kinachoelezwa kuwa amekuwa mwiba kwa
afisa elimu huyo, kutokana na Mkali kuwa na misimamo yake ya kazi hususani
katika kusimamia fedha na maendeleo ya elimu msingi wilayani humo.
Ngaga
analalamikiwa akidaiwa kufanya mchezo mchafu wa kuchota fedha za maendeleo ya
idara hiyo ya elimu, ambapo hata sasa walimu wengi wa wilaya hiyo wamekuwa
wakilalamika kutolipwa madai yao ya msingi ikiwemo fedha za uhamisho na
malimbikizo ya likizo.
Hata
hivyo hivi karibuni shilingi milioni 54,725,000 kutoka katika mfuko wa fedha za
ruzuku kwa ajili ya kuendeshea mitihani mashuleni (Capitation) Mkurugenzi huyo alichota
fedha hizo, kwa madai kuwa anaziazima na kwamba atazirejesha lakini baada ya
Afisa elimu Bw. Mkali kwenda kumtaka azirudishe ndipo alionekana kuwa mbogo
huku akiwa mkali na kumfokea.
Taarifa
zilizotufikia na kuthibitishwa na vyanzo mbalimbali vya habari kutoka ndani ya
halmashauri ya wilaya ya Mbinga, vimesema kuwa hata hivyo baada ya fedha hizo
kuonekana zinamletea shida huku akihofia kujibu hoja za ukaguzi na kukwepa
matatizo yanayoweza kujitokeza baadaye, aliamua kuchukua jukumu la kuzirejesha
haraka kwenye akaunti husika licha ya kukaa nazo muda mrefu, na wanafunzi mashuleni
wakikosa huduma za msingi.
No comments:
Post a Comment