Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, ACP Mihayo
Msikhela.
|
Na
Waandishi wetu,
Tunduru.
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida waendesha pikipiki maarufu kwa jina la yeboyebo,
wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma walifanya maandamano makubwa kwa lengo la
kupinga vitendo vya unyanyasaji ambavyo wanafanyiwa na askari polisi wa wilaya
hiyo, ikiwemo kuwakamata hovyo bila kufuata taratibu.
Madereva
hao waliandamana na kufanya fujo katika kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya
Tunduru, pia waandamanaji hao walichoma moto vibanda vinne ambavyo hutumiwa na
kampuni ya State business center na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
Kwa nyakati tofauti madereva hao walisema wamechukua maamuzi
hayo magumu, baada ya kuchoshwa na vitendo viovu ikiwemo kuombwa rushwa mara
kwa mara, ambavyo hufanyiwa na askari hao hasa wa kitengo cha usalama
barabarani.
Walisema
askari hao wamekuwa wakikaa katika maeneo ya vizuizi barabarani, ambavyo
hutumiwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kukusanyia ushuru wa halmashauri ya wilaya
hiyo ambapo huwakamata madereva hao kwa kutumia kamba zilizopo katika vizuizi
hivyo na kuwaamrisha kwa nguvu wawapatie fedha huku wakati mwingine wakiwa
hawana makosa.
Akizungumzia
tukio hilo Meneja wa kampuni ya State Bussiness center Sajidi Mchucha alisema
kuwa, katika tukio hilo waendesha pikipiki hao walichoma moto na kuteketeza
kabisa vibanda vyake vilivyojengwa katika maeneo ya barabara ziendazo na
kuingia mjini humo.
Mchucha
aliyataja maeneo hayo kuwa ni Mlingoti, Biasi, Tuleane na Mkapunda hali ambayo
imewatia hasara ya zaidi ya shilingi milioni 5 kwa kampuni yake pamoja na
kuteketeza vitabu vya kutunzia kumbukumbu za ofisi yake wakati anapofanya kazi
ya kukusanya ushuru.
Alisema
katika tukio hilo pia kijana wake wa kukusanya ushuru katika kituo cha Tuleane
Yazidu Nanyanga, amenusurika kuuawa baada ya madereva hao wa pikipiki kummwagia
mafuta ya petroli kwa nia ya kutaka kumchoma moto.
Kamanda
wa polisi mkoani Ruvuma, Mihayo Msikhela amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo
alisema tayari mlalamikaji amekwisha fungua kesi yenye namba TDR/IR/1058/2014
ambapo Jeshi la polisi linaitumia kufanya uchunguzi ikiwemo kuwakamata
waliohusika katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment