Askari aliyejeruhiwa na bomu mjini Songea mkoa wa Ruvuma, WP Mariamu Lukindo akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa huo iliyopo mjini hapa. |
Na
Mwandishi wetu,
Songea.
TIMU
ya makachero kutoka makao makuu ya Jeshi la polisi nchini, wakishirikiana na wa
mkoa wa Ruvuma, kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusiana na matukio ya mabomu yanayoendelea
kujitokeza mara kwa mara mkoani humo.
Makachero
hao wanatoka Jijini Dar es salaam, kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu
mmoja aliyelipukiwa na bomu maeneo ya majengo mjini songea na kujeruhi
askari polisi wawili, wakati akijiandaa kuwarushia askari waliokuwa doria
na kisha bomu hilo kumuua mwenyewe.
Hayo
yalisemwa na kaimu mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini, Naibu Kamishna wa
Jeshi la Polisi Diwani Athumani aliyewasili mjini Songea kwa helkopta kwa
ajili ya tukio hilo ambalo mtu ambaye hajatambulika, amelipukiwa na bomu
hilo na kufariki dunia papo hapo wakati akijaribu kuwarushia askari
waliokuwa doria na kujeruhi askari wawili.
Aliwataja
askari waliojeruhiwa kuwa ni PC Mselemu na WP Mariamu Lukindo ambaye bado
amelazwa katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Songea.
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aliyemtembelea majeruhi Mariamu Lukindo,
ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo ni la tatu kutokea mwaka huu mjini
hapa, likiwalenga askari polisi.
Nao
wananchi wanaoishi jirani na ulipotokea mlipuko wa bomu hilo, wameeleza
hofu waliyokuwa nayo baada ya mlipuko huo wa bomu na kuitaka serikali kufanya
jitihada ya kudhibiti hali hiyo ambayo inaendelea kuleta hofu kubwa kwa raia,
juu ya maisha na mali zao.
Mtu
mmoja ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka amefariki dunia baada ya
kulipukiwa na bomu huku utumbo wake ukiwa nje, na mkono wake kukatika alipotaka
kuwarushia askari hao.
Mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma alisema kuwa
watu wa nne waliokuwa na mtu huyo aliyekuwa akirusha bomu hilo, wamekimbia huku
polisi wakikamata simu za watu hao pamoja na ya marehemu huyo.
Mwambungu alisema kukamatwa kwa simu
hizo ni mwanzo mzuri wa kuwabaini walipuaji mabomu kwa askari polisi mjini
Songea.
No comments:
Post a Comment