JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
ANUANI YA SIMU: POLISI
RUVUMA
NAMBARI YA SIMU 025-26 KAMANDA WA POLISI 025-2602266 MKOA WA RUVUMAFAX NO. 025-2600380 S.L.P.19,
SONGEA.
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
MTU MMOJA AMEFARIKI KWA IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI
RUVUMA
Mnamo tarehe 22/09/2014 majira ya saa
kumi na moja jioni huko mtaa wa Ruvuma manispaa ya Songea Emeresiana Goliama
(70), Mngoni, Mkristo na mkazi wa Ngahokola amefariki dunia wakati akipelekwa
hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu, baada marehemu na wana ukoo wenzake
wapatao kumi, kwenda kwa mganga wa kienyeji maarufu kwa jina la Angaza
aliyewaambia kuwa kati yao wanne ni wachawi akiwemo marehemu walinyolewa nywele
na kunyweshwa dawa kitendo kilicho pelekea hali ya Emeresiana kubadilika ghafla.
Wanaukoo hao walifikia uamuzi wa
kwenda kwa mganga baada ya kukaa kikao na kujadili matatizo ya ukoo wao ikiwa
ni pamoja na kupata kichaa na ugonjwa wa kifafa, hivyo mganga aliwataja watu
wanne kuwa ni wachawi 1. Meresiana Goliama, ambaye ndiye marehemu 2. Oruban
Goliama, (75), mkulima, Mkristo, Mngoni na mkazi wa Ngahokola 3. Nikola
Huma, (68), mkulima Mristo na mkazi wa Ngahokola 4. Razaria Matembo,
(64), Mkristo, Mngoni, mkulima na mkazi wa Ngahokola.
Kufuatia hali hiyo Jeshi la Polisi
Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watu watatu 1. Daudi Goliama (49), Mngoni,
Mkristo na mkazi wa Ngahokola 2, Samson Goliama (40), Mngoni, Mkristo na
mkazi wa Ngahokola wote hao wanamuita marehemu shangazi na 3. Rafael
Goliama (29), Mngoni, Mkristo na mkulima wa Ngahokola ambaye ni mjukuu wa
marehemu, kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha kufuatia hali hiyo wananchi
wanatakiwa kutojihusisha na imani za kishirikina ambazo mwisho wake zinapelekea
kupoteza maisha na chuki kwa jamii.
No comments:
Post a Comment