Nyandindi)
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
TUNAISHI kwa taabu serikali
haitujali au kwasababu sisi tunaishi mpakani, miundombinu ya barabara kutoka
Mbinga mjini kuja huku ni shida tupu, kilio chetu ni huduma za afya, maji na
barabara.
Haya ndiyo maneno ya wakazi wa
kijiji cha Lunyere kitongoji cha Darpori, wanaoishi katika kijiji hicho ambacho
kipo umbali wa kilometa 98 kutoka Mbinga mjini.
Kijiji hicho kipo mpakani ambapo
kinapakana na nchi ya Msumbiji upande wa Kusini na maisha kwenye kijiji hicho
ambacho kipo mbali kuliko vyote katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ,
wananchi wake ni mchanganyiko wa makabila mbalimbali ambao hujishughulisha na
kilimo, ufugaji, biashara na uchimbaji wa madini aina ya dhahabu.
Wakazi katika kijiji cha Lunyere
wapo jumla 6060 Wanaume 3039 na Wanawake 302, hawana kituo cha kutolea huduma
za afya, barabara zimekuwa mbaya na huduma ya maji kwao imekuwa ni shida.