Wanafunzi
wa darasa la awali shule ya msingi Masumuni iliyopo wilayani Mbinga
mkoa wa Ruvuma, wakiwa wamepanga foleni kwenda kupokea uji kwa ajili ya
kifungua kinywa majira ya asubuhi kama walivyokutwa na mpiga picha wetu.
Serikali hapa nchini imekuwa ikisisitiza shule nyingi kutoa huduma ya chakula kwa wanafunzi mashuleni ili waweze kuondokana na njaa na hatimaye wafanye
masomo
yao vizuri. (Picha na Kassian Nyandindi)
Na Dustan Ndunguru,
Songea.WANAFUNZI na walimu wa shule ya msingi Sokoine kijiji cha Ngadinda Songea vijijini mkoani Ruvuma, wanalazimika kujisaidia vichakani kutokana na uhaba wa vyoo uliopo shuleni hapo.
Shule hiyo inakabiliwa na changamoto
nyingi kutokana na uchanga wake, hivyo jitihada za kuinusuru ili iweze
kuondokana na matatizo hayo zinahitajika kwa uharaka zaidi ili wanafunzi na
walimu wasipatwe na magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Theoderi Moyo alisema, mahitaji halisi ya matundu ya vyoo ni 16 na sasa shule ina matundu manne tu ambayo hayatoshelezi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Theoderi Moyo alisema, mahitaji halisi ya matundu ya vyoo ni 16 na sasa shule ina matundu manne tu ambayo hayatoshelezi.
Kutokana na hilo walimu wamekuwa
wakijisaidia katika vyoo vya nyumba za watu wanaoishi jirani na shule hiyo.
Alisema licha ya kufanya vikao
mbalimbali ambavyo vilijumuisha wazazi na walimu bado suala hilo limekuwa gumu katika
utekelezaji hivyo jitihada zinahitajika zaidi katika kutatua suala hilo.
Alieleza kwamba uongozi husika wa
Halmashauri ya wilaya ya Songea umekwisha pelekewa taarifa, lakini hadi sasa
hakuna utekelezaji au hatua zilizochukuliwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Ngadinda Bw. John Komba alisema, tatizo kubwa lililopo katika kijiji chao ni ubishi wa baadhi ya wananchi kutoshiriki katika shughuli za maendeleo hususani kwa kazi za kujitolea.

Bw. Komba alifafanua kuwa Kutokana
na hali hiyo wanakusudia kutumia sheria ndogo ndogo zilizowekwa na serikali ya
kijiji hicho, ili kuwabanaa wale wote wasiokuwa tayari kushiriki katika
maendeleo.
No comments:
Post a Comment