Na
Steven Augustino,
Tunduru.
MADIWANI
wa viti maalumu katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wameomba kuridhia na kuruhusu kufunguliwa
kwa wodi mpya iliyojengwa katika hospitali ya Wilaya hiyo kwa ajili ya kujifungulia akina Mama wajawazito, wanaoenda kupata huduma hiyo muhimu hospitalini hapo kwa kuanza.
Kilio
hicho kilianza kuwasilishwa na Diwani wa Viti maalumu wa Tarafa
ya Matemanga Stawa Omari huku akiungwa mkono na Swema
Kalipungu wa Tarafa ya Mlingoti na Alus Yunus wa Nalasi walisema hivi sasa hali ya akina mama hao ni tete kutokana na wengine hujifungua wakiwa wamelala chini sakafuni.
Madiwani
hao walisema kuna
wakati akina mama wajawazito wamekuwa wakijifungulia katika chumba cha kupokelewa wagonjwa.
Walidai
kuwa imefikia hatua wakati mwingine hata wagonjwa wanaoenda kupata matibabu
hospitalini hapo hupata shida pale wanapohitaji
huduma za vipimo choo ndogo na kubwa ambapo hulazimika kwenda vyoo vya nyumba
za jirani kutokana na miundo mbinu ya hospitali hiyo kutotosheleza.
Walisema
kila wanapohitaji maelezo kwa wataalamu husika wamekuwa wakiambiwa
kuwa tatizo linalo wa kwaza ni kutokana na wodi
hizo mpya kutokamilika miundo mbinu husika.
Aidha
madiwani hao waliendelea kuiomba halmashauri
kutenga eneo jingine la kujifungulia akina mama,
ambao wanaenda kujifungua katika hospitali hiyo kujisitiri mahali pa zuri.
No comments:
Post a Comment