Na Steven Augustino,
Tunduru.
KATIBU wa Siasa na ushirikiano wa kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt. Asha Rozi Migiro ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, kwa kuanza kwa kasi utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule mbalimbali za sekondari wilayani humo, ikiwa ni juhudi ya serikali ya awamu ya nne kuinua taaluma kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi.
Dkt. Migiro ambaye amefuatana na Katibu mkuu wa CCM
taifa Abrahaman Kinana alisema hayo wakati alipokuwa
katika shule ya sekondari ya kutwa, Mgomba sekondari iliyopo kata ya Majengo wilayani
humo.
Alisema huo ni mpango ambao umewekwa na serikali katika kuhakikisha wilaya husika vyumba vya maabara vinajengwa katika shule ili kuinua kiwango cha taaluma katika masomo ya sayansi kwa wanafunzi.
Ujenzi huo unaenda sambamba na nyumba za walimu, nayo
imekuwa ni kero kubwa hususani kwa shule zilizopo vijijini.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa maabara ya shule hiyo
kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bw. Robart
Nehatta, ambapo mkuu wa shule hiyo Elis Banda alimweleza Dkt. Migiro na msafara
wake kuwa mradi wa ujenzi huo unatekelezwa kupitia mpango wa Maendeleo ya
Elimu ya Sekondari(MMES II) katika mwaka wa fedha 2012/2013.
No comments:
Post a Comment