Na Mwandishi wetu,
Dar es Salaam.
KITENDO cha Katibu
mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye cha kupinga uteuzi wa
Mawaziri uliofanywa na Mwenyekiti wa chama hicho ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ni mwendelezo wa tabia zake za ukosefu wa nidhamu kwa viongozi wake.
Hayo yamo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
aliyoitoa hivi karibuni, ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es
salaam, John Guninita amesema Nape ni
mkiukwaji wa maadili, asiyeheshimu wakubwa ambao wamemteua kushika nafasi hiyo.
Alisema ni kiongozi ambaye anatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka yake hivyo ni vema akafahamu
kuwa madaraka ya kuteua Baraza la mawaziri ni kazi ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano na sio vinginevyo.
Guninita alisema hata kama ingetokea Rais akashauriwa
na washauri zaidi ya mia moja, bado uamuzi wake unapaswa kuheshimiwa na hakuna
mtu anayeweza kuingilia au kubeza.
Alisema kitendo
cha Nape kutoa maneno ya dhihaka ni mwendelezo wa tabia zake za kuropoka na
kujitwalia madaraka makubwa zaidi ya mwenyekiti au katibu wa CCM Taifa.
"Yote yaliyotamkwa na Nape kwenye mkutano wake na
waandishi wa habari hivi karibuni ni mawazo yake binafsi na sio ya chama kwani
hakuna kikao chochote kilichokaa na kumtuma akaongee mambo haya”, alisema.
Guninita alimtaka Nape kuacha kuwaita wenzake kuwa ni mizigo, badala yake ajitazame kwanza yeye mwenyewe kama ni msafi ndani ya chama hicho au la kutokana na kile alichoeleza kuwa amekuwa akikiyumbisha chama kutokana na kauli zake.
Guninita alimtaka Nape kuacha kuwaita wenzake kuwa ni mizigo, badala yake ajitazame kwanza yeye mwenyewe kama ni msafi ndani ya chama hicho au la kutokana na kile alichoeleza kuwa amekuwa akikiyumbisha chama kutokana na kauli zake.
No comments:
Post a Comment