Na Steven Augustino,
Tunduru.
WANACHAMA na wakereketwa wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Majengo wilayani Tunduru Ruvuma, wamehimizwa kudumisha muungano na upendo miongoni mwao na kuhakikisha wanapata ushindi wa chama chao katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Mariwani Athumani Nkinde wa Kata hiyo na Diwani waviti
maalumu wa tarafa ya Mlingoti Bi. Atingala Mohamed walisema hayo kwa nyakati
tofauti wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi ya bomba ugawaji
wa vifaa vya kutengenezea Batiki, mafuta ya kupaka, sabuni za maji, na vipande
katika kata hiyo.
Madiwani hao walisema kuwa endapo wanaCCM hawatashikamana katika ujenzi na uimarishaji wa chama chao ipo hatari ya mamluki kuingia miongoni mwao, na kuwavuruga kwa lengo la kuvipatia ushindi vyama pinzani.
Akifafanua taarifa ya ujenzi wa mtandao wa bomba la maji hayo
na vifaa hivyo Diwani Athuman Nkinde, alisema kuwa hadi kukamilika kwake miradi
hiyo imegharimu shilingi 400,000 na akatumia nafasi hiyo kuwaomba waitumie na
kuitunza.
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita diwani huyo ametekeleza ahadi za kuanzisha miradi ya kuuza Kuni na mkaa unaosimamiwa na viongozi wa kata hiyo, mradi wa kilimo cha mpunga unaosimamiwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Kata hiyo.
No comments:
Post a Comment