Akina mama wa mkoa wa Ruvuma, wakiendelea kwa pamoja kufurahia maadhimisho ya sherehe za siku ya mwanamke Duniani. |
Joseph Mkirikiti Mkuu wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, akipokea maelezo mafupi kutoka kwa mjasiriamali ambaye anatengeneza kinywaji cha asili aina ya "Wine". {Picha zote na Gwiji la matukio Ruvuma} |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
WANAWAKE
mkoani Ruvuma wamelalamikia na kupinga vikali
vitendo vinavyoendelea kushamiri, ambavyo hufanyiwa miongoni mwao mkoani humo
ikiwemo ukatili, kupigwa na kuuawa kutokana na hisia za kimapenzi.
Aidha
wamesema kuwa upande wa watoto wa kike kumekuwa na ukosefu wa usawa katika
kupata elimu, hivyo kusababisha watoto wengi kuishi katika mazingira hatarishi.
Kilio
hicho kilitolewa na Wanawake hao kupitia risala yao iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa
wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti, katika sherehe za maadhimisho ya kilele cha
siku ya wanawake duniani kilichofanyika katika mkoa huo kijiji cha Kihereketi
kata ya Nyoni wilayani Mbinga.
Akisoma
taarifa hiyo kwa niaba ya wanawake wenzake, Cosma Mbawala ambaye ni mkazi wa kijiji
hicho alisema wanawake ni kichocheo kikubwa katika harakati za kuleta maendeleo
lakini inasikitisha kuona wamekuwa wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao za
msingi.
Mbawala
alifafanua kuwa kundi hili limekuwa pia likitengwa katika kushiriki kwenye
maamuzi mbalimbali, ikiwemo uwiano na ugawanaji sawa wa rasilimali muhimu.
Alisema
katika kukabiliana na matatizo hayo, ni wakati sasa kwa serikali kutupia jicho
namna ya kupambana na hali hiyo ili kumpunguzia mzigo mwanamke na kumpa muda
zaidi wa kushiriki katika kupanga na kusimamia mipango ya kimaendeleo.
“Serikali
isimamie na kukemea vitendo viovu vinavyofanyika katika jamii hasa
udhalilishaji kama vile ubakaji, unyanyapaa na
ukatili wa aina nyingine ambao tunafanyiwa dhidi yetu”, alisema.
Hata
hivyo kwa upande wake Mgeni rasmi wa sherehe hizo Mkirikiti aliiasa jamii
iachane na vitendo hivyo vya ukatili kwa kuhakikisha kwamba, haki sawa kwa
mwanamke zinazingatiwa huku akilinyoshea kidole kundi la Wanaume ambalo ndilo
kinara wa vitendo hivyo.
Mkirikiti
alisema ni vyema jamii ikaona umuhimu wa thamani ya mwanamke ikiwemo
kuwashirikisha katika mambo muhimu ya kimaendeleo hususan elimu na sio
kuwatenga au kufanya ubaguzi kwa namna moja au nyingine.
No comments:
Post a Comment