Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu. |
Na Kassian Nyandindi,
Ruvuma.
MKUU wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, leo ameanza ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali wilayani Nyasa na ifikapo Marchi 25 mwaka huu, ataendelea wilayani Mbinga.
Huo ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi hapa mkoani Ruvuma.
Akiwa katika wilaya hizo Mwambungu atapokea taarifa za maendeleo ya wilaya hizo, kuongea na wananchi na kukagua miradi mbalimbali kama vile barabara, mashamba ya kilimo cha mahindi, skimu za kilimo cha mpunga na zahanati.
Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka wilayani Nyasa, zinaeleza kuwa Mkuu huyo wa mkoa amelalamikia ujenzi wa barabara za wilaya hiyo kwa kiwango cha chini jambo ambalo linadhihirisha kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Pia amezitaka mamlaka husika hususan watendaji wa wilaya hiyo kufanya kazi kwa weledi na kufuata misingi ya utawala bora kama sheria za nchi zinavyotaka.
No comments:
Post a Comment