Na Steven Augustino,
Tunduru.
JESHI la polisi wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, limeagizwa kuhakikisha kwamba linafanya uchunguzi
wa kina na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu walioshiriki katika zoezi
la hujuma za kubomoa jengo la mradi wa Ushoroba na kuisababishia serikali
hasara ya zaidi ya shilingi milioni 36.9.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho alitoa agizo hilo katika kikao cha
kamati ya ulinzi na usalama, kilichoketi kwa ajili ya kujadili hasara za uharibifu
wa mradi huo, ambao unajengwa kijiji cha Lukala kilichopo Kata ya Mchesi tarafa
ya Lukumbule wilayani humo.
Alisema mradi huo unafadhiliwa na nchi ya Ujerumani,
unajengwa ikiwa ni juhudi ya mwendelezo mradi wa ushirikiano wa kudhibiti vitendo
vya ujangili, ambao umekuwa ukifanywa na wawindaji haramu katika nchi za Tanzania na
Msumbiji.
Taarifa za utekelezaji wa mradi huo zitahusisha ujenzi
wa nyumba moja na ofisi, itakayotumiwa na maafisa watakaoshiriki katika zoezi
la ulinzi na uzuiaji wa wawindaji haramu na kwamba fedha hizo zimetolewa
serikali ya ujenrumanin kwaajili ya kifanikisha zoezi hilo.
Naye Mbunge wa Tunduru Kusini Alhaji Mtutura alisema
kuwa baada ya kubaini kuwepo kwa hujuma na uharibifu huo, alimuamuru mkandarasi
anayejenga majengo ya nyumba ya kuishi watumishi unaogharimu shilingi milioni
19,746,500 na ofisi itakayotumiwa na maafisa hao itakayogharimu shilingi
milioni 17,195,562 hadi kukamilika kwake kusimamisha ujenzi huo hadi atakavyo
taarifiwa.
Alisema awali mradi huo ulipangwa kujengwa katika kijiji
cha Wenje mpakani mwa nchi za Msumbiji na Tanzania, eneo ambalo wananchi wake
waliukataa na baada ya kukaa vikao vilivyowashirikisha wananchi hao,
ilikubaliwa ujengwe katika kijiji cha Lukala lakini inashangaza wao kuukataa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika
kijiji hicho zinaeleza kuwa majengo hayo, yalibomolewa na kundi la vijana zaidi
ya 100 wanadaiwa kuwa walishawishiwa na kundi la wawindaji haramu, ambao
wanadaiwa kuendelea kuwashawishi wananchi wa kijiji hicho, wasiukubali mradi
huo kwa madai kwamba wakizubaa na kuacha mradi huo uendelee, wananchi hao
hawatafanya shughuli zozote za kibinadamu katika mapori hayo.
No comments:
Post a Comment