Na Steven Augustino,
Tunduru.
KATA ya Namasakata wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, wametishia kutoa kafara ya mtu achinjwe, kwa
ajili ya tambiko litakalosadia wananchi wa kata hiyo, kupata huduma ya maji safi na salama.
Diwani wa kata hiyo Masache Ally alisema hayo mbele ya
Mkuu wa wilaya hiyo Chande Nalicho, kufuatia adha kubwa wanayopata wananchi
wake juu ya upatikanaji wa maji safi
na salama.
Alisema wamechoshwa na danadana na ahadi hewa
zinazotolewa na serikali juu ya utekelezaji na utatuzi wa tatizo hilo.
“Sisi wananchi wa kata ya Namasakata tumejiandaa na
tuko tayari kumtoa hata mtu mmoja miongoni mwetu ili auawe kwa kuchinjwa, na
damu yake imwagike na kutumika kama kafara itakayofanikisha kupatikana kwa maji
na kuwaondolea kero wananchi wa kata hii”, alisema.
Masache alisema kuwa mbali na vijiji vilivyopo katika
kata yake kushirikiana na wataalamu katika utafiti wa jambo hilo, lakini wameishia kuahidiwa kupatiwa kupelekewa
miradi ya maji miaka mingi iliyopita, na hakuna utekelezaji uliofanyika mpaka sasa.
Wakizungumzia hali hiyo Mwenyekiti wa kijiji cha Namasakata
Yusuf Mkali na mkazi wa kijiji cha
Mkasale Nuru Hassan walisema kuwa vijiji hivyo, vinakabiliwa na hali mbaya ya
upatikanaji wa maji tangu mwaka 1982 kiasi cha kutishia maisha ya wakazi wake.
Walisema upande wa kijiji cha Mkasale hali ni mbaya
zaidi kutokana na kuwepo kwa shubiri, ambayo huwapata akina mama wanaokwenda
kujifungua katika kituo cha afya ambapo hulazimika kwenda kuchota maji mtoni
umbali wa zaidi ya kilometa mbili, huku wakiwa katika hatari ya kujeruhiwa ama
kuuawa na wanyama wakali ambao pia huyatumia maji hayo kunywa.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho alimtaka Mhandisi
wa idara ya maji wilayani humo Paschal
Kidiku kushirikiana na wataalamu kufanya utafiti, na kutoa majibu ya uhakika
kwa wananchi hao, ili wajue na kutoa maamuzi ya kukihama kijiji chao au la.
No comments:
Post a Comment