Na Kassian Nyandindi,
Ruvuma.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limesema
Serikali kamwe haitavumilia kuona askari wake wamekuwa wakijihusisha na vitendo
vya uhalifu, badala yake itahakikisha kwamba inachukua hatua mara moja kwa yule
anayekiuka maadili ya utumishi wa umma ili kuwafanya wananchi na mali zao
wanaishi katika hali ya usalama.
Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi
wa mkoa huo Akili Mpwapwa alipokuwa katika ziara yake ya kikazi akizungumza na
askari polisi na wadau mbalimbali wa mkoa wa Ruvuma, kwa lengo la kusisitiza
juu ya uimarishaji wa ulinzi shirikishi.
Mpwapwa alisema lengo la ziara hiyo ni
kutaka kutambua maeneo yake ya kazi, kubaini uhalifu, vikundi vya ulinzi
shirikishi na wadau ambao wamekuwa wakichangia jeshi la polisi katika kuleta
ufanisi wa masuala ya ulinzi katika maeneo yao.