Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Ernest Kahindi, akiwa ofisini kwake wilayani humo. (Picha na Kassian Nyandindi) |
Na Kassian Nyandindi,
Nyasa.
SAKATA la mgogoro wa
kugombea ardhi na mipaka katika kitongoji cha Mshangano kijiji cha Liparamba
tarafa ya Mpepo wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, limechukua sura mpya kufuatia
Wakazi wa maeneo hayo kumlalamikia Mkuu wa wilaya hiyo Ernest Kahindi huku
wakimnyoshea kidole kwamba ameshindwa kumaliza mgogoro huo kwa kufuata taratibu
husika ikiwemo ridhaa ya wananchi, badala yake anatumia nguvu kubwa
kunyanyasa viongozi wa kijiji hicho.
Wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti kijijini hapo, wakazi hao
walisema Kahindi amefikia hata hatua ya kumweka mahabusu kwa siku tatu katika
kituo kikuu cha polisi wilaya ya Nyasa, Mwenyekiti wa kijiji Joseph Komba bila
kosa lolote huku akizuia dhamana.
Uchunguzi umebaini
kuwa Mwenyekiti huyo aliwekwa mahabusu kuanzia siku ya Ijumaa Juni 20 na
kudhaminiwa Juni 23 mwaka huu majira ya jioni, ambapo kufikia saa 11 jioni siku
hiyo ndipo alichukuliwa maelezo na kuambiwa atafute mtu wa kumdhamini huku
akipewa usumbufu wa kuendelea kuripoti kila siku katika kituo hicho cha polisi.
Kadhalika Mkuu wa
Polisi wilaya ya Nyasa (OCD) Amiri Mganga alipopigiwa simu ili aweze
kuzungumzia hali hiyo alikiri kushikiliwa kituoni hapo Mwenyekiti huyo na
kusema; “hivi sasa siwezi kuzungumzia lolote nimebanwa na kazi nipo bize kidogo
nipigie muda mwingine, na kuishia kukata simu".
Taarifa zinaeleza
kuwa kuwekwa mahabusu kwa Mwenyekiti Komba kunatokana na kujenga msimamo wake wa
kutotaka kugawa ardhi na mipaka ya kijiji bila kufuata taratibu husika, hivyo
kuonekana kuwa mwiba kwa Mkuu huyo wa wilaya ya Nyasa.
Imeelezwa kuwa mtu
ambaye anazua mgogoro huo wa ardhi na mipaka katika kijiji cha Liparamba,
ni Mwanajeshi mstaafu Florian Geuza ambaye alipoulizwa alisema kuwa maeneo
anayoyadai ni ya kwake, familia yake na ndugu zake.
Geuza alisema yeye
eneo hilo analolidai kijijini hapo linazaidi ya ekari 300 ambapo aliachiwa
urithi na baba yake mzazi miaka mingi kabla hajafariki dunia.
Katika hatua nyingine
kwa upande wao wananchi walisema kitendo hicho kinachofanywa na Mkuu huyo wa
wilaya ya Nyasa hakipaswi kuvumiliwa hata kidogo, hivyo wanaiomba serikali
kuingilia kati ili kuweza kuepusha na kunusuru kutokea kwa mauaji ya kugombea
ardhi na mipaka, kati ya wananchi wa kitongoji hicho na Mwanajeshi huyo
mstaafu.
Walieleza kuwa ni
jambo la kusikitisha kwa kiongozi wa ngazi ya juu kutumia nguvu na unyanyasaji
kwa viongozi wa maeneo hayo, wakati wenye maamuzi ya ugawaji wa maeneo ya
kijiji ni wananchi wenyewe kupitia vikao halali vilivyoketi kisheria na sio
vinginevyo.
Walisema kuwa mgogoro
huo wa kugombea mipaka umedumu kwa miaka mitatu sasa, licha ya viongozi husika
kuwa na taarifa juu ya tatizo hilo lakini kila kukicha kumekuwa ukifanyika
mchezo mchafu ambao huzalisha matatizo yenye kuhatarisha misingi ya amani
katika kijiji cha Liparamba.
Walifafanua kwamba
hali hiyo inatokana tu na mstaafu huyo wa JWTZ kuvamia maeneo ya wananchi hao
na kusema kuwa ni ya kwake anayamiliki tokea mwaka 1952 jambo ambalo linazua
utata kila kukicha.
Pamoja na
kutoa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kuanzia kwenye
ngazi ya kata na wilaya, walisema bado hakuna dalili zinazoonesha kuzaa matunda
badala yake muda mwingi viongozi wa wilaya hiyo wamekuwa wakiegemea upande wa
Mwanajeshi huyo.
“Hali hii
inasababisha tuishi kwa hofu na mashaka juu ya jambo hili, hasa pale
tunapolazimika kwenda kwa ajili ya uzalishaji wa mazao yetu shambani”, alisema
Sikitu Kawago mkazi wa kijiji cha Liparamba.
Naye mkazi mmoja wa kijiji hicho Lucas Ngonyani alisema kama uongozi wa wilaya hiyo utaendelea kufumbia macho tatizo hilo, kuna uwezekano wa kuwepo kwa mapigano na kusababisha umwagaji wa damu.
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Liparamba Denice Manyahi alipohojiwa ofisini kwake alikiri kuwepo kwa hali ya sintofahamu ya kugombea ardhi na mipaka, huku akisema tayari hali imekuwa mbaya kiasi ambacho inatakiwa hatua za busara zenye kufuata misingi na taratibu za kisheria ifuate ili kuweza kuleta amani kijijini hapo.

Manyahi alieleza kuwa
hali hii inatokana na uzembe husika unaofanywa na viongozi wachache wilayani
Nyasa, hivyo huenda tatizo hilo lisipotatuliwa kwa uharaka inaweza kutokea
maafa makubwa ambayo baadaye kuigharimu serikali.
Naye Ofisa mtendaji wa kata ya Liparamba Philemon Ngaponda alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi, alithibitisha kuwepo kwa mgogoro wa kugombea ardhi na mipaka huku akiongeza kwamba taratibu husika zimeanza kuchukulia ili kuweza kumaliza tatizo hilo.
“Ni kweli mgogoro upo tunachosubiri ni maamuzi ya viongozi wa ngazi ya juu, mimi siwezi kuzungumzia sana juu ya jambo hilo tusubiri maamuzi yatakayotolewa”, alisema Ngaponda.

Mkuu wa wilaya ya
Nyasa Kahindi alipoulizwa juu ya tatizo hilo la wananchi wa kijiji cha
Liparamba wilayani humo, alisema hawezi kuzungumzia lolote kwa sasa huku
akiongeza kuwa linashughulikiwa kisheria.
Hata hivyo
alipotakiwa kutolea ufafanuzi wa malalamiko ya kunyanyasa viongozi wa kijiji
hicho alisema; “nimekuambia naomba uvute subira Nyandindi, hili suala
linashughulikiwa kisheria utapata taarifa kamili kwa sasa siwezi kuzungumzia
lolote”.
No comments:
Post a Comment