Na Kassian Nyandindi,
Ruvuma.
BAADA ya siku
chache kupita kufuatia tukio la nani amefanya kitendo kiovu cha kurusha bomu la
kienyeji katika mtaa wa Msufini Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, na kujeruhi
baadhi ya askari Polisi mjini hapa, Mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu amekutana
na waendesha pikipiki wa manispaa hiyo na kuwataka kujenga ushirikiano
ili kuweza kulinda amani ya nchi dhidi ya maadui ambao hawalitakii mema taifa hili.
Mwambungu
amekutana leo na madereva hao maarufu kwa jina la “Boda boda” katika ukumbi wa
Songea Club uliopo mjini Songea, akisisitiza kujenga ushirikiano kwa vyombo vya
usalama ili kuweza kupata ukweli wa tukio hilo na kuwafanya wakazi wa mji huo,
watu wengine (wageni) wanaoingia na kutoka kuondoa hofu na kuishi katika hali
ya usalama.
Akizungumza kwa
njia ya simu na mwandishi wa habari hizi, Mkuu huyo wa mkoa alisisitiza kuwa
jamii ihakikishe kwamba amani utulivu vinatawala miongoni mwao, na pale wanapoona
kuna sintofahamu ni vyema watoe taarifa katika vyombo husika vya usalama ili
kuweza kubaini uhalifu unaofanyika na hatua ziweze kuchukuliwa haraka dhidi ya
wahalifu.
“Ni kweli leo
nimezungumza nao, ni kawaida yangu kukutana nao jambo kuu nimesisitiza kujenga
ushirikiano na amani, na waache kutumiwa katika mambo ya kisiasa, siku
zote amani ndio msingi mkuu”, alisema Mwambungu.
Mwambungu
aliongeza kuwa hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi
juu ya tukio hilo, na kwamba mpaka sasa hakuna mtu aliyepatikana ambaye
anahusika kutenda unyama huo.
Pamoja na mambo
mengine tukio la kurushwa kwa bomu hilo, lilitokea Septemba 16 mwaka huu majira
ya 1:25 usiku katika mtaa wa Msufini katika Manispaa ya Songea na kuwajeruhi
askari Polisi watatu kati ya w anne waliokuwa doria huku Jeshi la Polisi nchini
likithibitisha kuwa bomu hilo limetengenezwa kienyeji.
Askari
waliojeruhiwa ni G 5515 PC John, G 7351 PC Ramadhan na WP 10399 Felista ambapo
baada ya kujeruhiwa kwa bomu hilo, walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya matibabu zaidi.
PC John aliyepata majeraha kiasi alipatiwa matibabu siku hiyo na kuruhusiwa, huku askari wawili PC Ramadhan na WP Felista wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
PC John aliyepata majeraha kiasi alipatiwa matibabu siku hiyo na kuruhusiwa, huku askari wawili PC Ramadhan na WP Felista wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment