Na Steven
Augustino,
Lindi.
WAANDISHI wa habari Nyanda za juu kusini, wameshauriwa
kufanya utafiti na kuandika habari zitakazofichua vitendo viovu vinavyofanywa
na baadhi ya vigogo hapa nchini, ambao wamekuwa wakifanya biashara ya uvunaji
misitu na kusafirisha kwa njia za panya jambo ambalo limekuwa likiikosesha
serikali mapato yake.
Meneja kampeni ya mama misitu, Gwamaka Mwakyanjala alisema
hayo alipokuwa akitoa mafunzo ya siku tano kwa waandishi wa habari wa mikoa ya
Ruvuma, Mtwara na Lindi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Lindi
mkoani hapa.
Mwakyanjala alifafanua kuwa lengo la mafunzo hayo, ni
kuwajengea uwezo waandishi wa mikoa hiyo waweze kuandika habari za misitu ili
kusaidia kuibua mijadala ambayo itaiwezesha serikali, kutatua kero ambazo
zimekuwa zikijitokeza juu ya uvunaji haramu wa misitu.
Alisema waandishi wa habari wanapaswa kuisaidia jamii na
wadau wa misitu ili kuweza kuilinda, kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa
katika kuilinda kutotekelezwa ipasavyo.
Awali akifungua mafunzo hayo, Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri
ya Lindi Suleiman Ngaweje aliwataka waandishi wa habari kutumia mafunzo
watakayopata kutoa taarifa mbalimbali za misitu kwa wananchi, ikiwemo pia
matumizi endelevu ya misitu ili wananchi waweze kunufaika nayo.
“Waandishi wa habari nawaomba mkawe mabalozi wazuri kwa
kuwaeleza wananchi manufaa ya misitu na matumizi endelevu, misitu ni mali yetu
tuitunze ili iweze kutusaidia kupata kipato na kukuza maendeleo yetu”, alisema
Ngaweje.
No comments:
Post a Comment