Na Steven Augustino,
Tunduru.
WILAYA ya Tunduru mkoani Ruvuma imeanza kutekeleza mpango wa kuwapatia chanjo mpya ya kuzuia ugonjwa vichomi na kuharisha kwa kuwapatia chanjo hiyo jumla ya watoto 12,372 walio chini ya umri wa mwaka mmoja ikiwa ni juhudi ya serikali kupambana na vifo vitokanavyo na magonjwa hayo.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho alisema hayo alipokuwa akizundua chanjo hizo katika ukumbi wa kutolea huduma ya mama na mtoto hospitali ya serikali ya wilaya hiyo iliyopo mjini hapa.
Katika hilo Nalicho aliwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao bila kukosa, ili wapatiwe chanjo hizo zikiwa ni juhudi za mapambano dhidi ya magonjwa hayo.
Alisema endapo kutatokea wazazi na walezi kuzembea katika kuzingatia kupeleka watoto wao kupatiwa chanjo ya magonjwa hayo kunaweza kusababisha vifo vingi visivyo vya lazima.
Alisema watoto wenye umri chini ya miaka mitano ndiuo ambao wamekuwa wakishambuliwa na magonjwa hayo hivyo kuna kila sababu mzazi kuzingatia hili ili kuepukana na matatizo au madhara yasiyo ya lazima.
Awali akitoa taarifa ya chanjo hizo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt. Bernad Mwamanda alisema, kati ya watoto hao watakaopatiwa chanzo hizo watoto chini ya miaka mitano katika wilaya hiyo ni 53,065.
Dkt. Mwamanda aliendelea kubainisha kuwa watoto Chini ya mwaka mmoja waliopagwa kupatiwa chanjo hizo pia ni 11,344 na akatumia nafasi hiyo kuwatoa mashaka wazazi wa watoto hao, kwamba chanjo hizo ni salama na zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) kuwa hazina madhara.

Akizungumzia takwimu za magonbjwa hayo Dkt. Mwamanda alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2011 jumla ya watoto 78 walipoteza maisha kutokana na magonjwa hayo kati ya watoto 35,033 waliolipotiwa kuugua magonjwa hayo.
Akizungumzia utekelezaji wa zoezi hilo msimamizi wa huduma za afya ya mama na mtoto katika Kuruthum Mnyanga alisema kuwa jumla ya wahudumu 98 wamekwisha patiwa mafunzo kwa ajili ya kuleta ufanisi wa zoezi hilo.
Kwa nyakati tofauti wakizungumzia hilo baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa wa chanjo hiyo, Joyce Paul na Mwanahawa Salum waliipongeza serikali kwa kubuni na kuleta chanjo hiyo ambayo walidai kuwa itawasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya watoto wao.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma Dkt. Daniel Malekela alisema mkoa huo unatarajia kutoa chanjo hizo kwa zaidi ya watoto 53,000 wenye umri chini ya miaka mitano.

Wakati taarifa hizo zikitolewa, takwimu za magonjwa hayo zinaonesha kusababisha watoto takribani 6,000 kupoteza maisha kila mwaka na kushika nafasi ya pili na ya tatu kwa kusababisha vifo vingi vya watoto yakitanguliwa na Malaria.
No comments:
Post a Comment