Monday, January 14, 2013

WILAYA YA TUNDURU YATOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI SERIKALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

  
Hii ndio adha iliyopo katika barabara ya kwenda Tunduru mkoani Ruvuma, serikali mmeliona hili, kama tumeliona sasa kilio cha wananchi hawa kifanyiwe kazi haraka ni miaka mingi sasa imepita hali bado ni tete hasa katika kipindi cha masika.(Picha na Steven Augustino)





Na Steven Augustino, 
Tunduru.
 
VYOMBO vya habari nchini vimehimizwa kufuatilia na kuandika habari za maendeleo, changamoto na matatizo yote yanayowasumbua wananchi waishio vijijini hususani pembezoni mwa wilaya husika. 

Hayo yalisemwa na mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho wakati akitoa taarifa ya utekeelezaji wa Serikali ya awamu ya nne kupitia
Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2005 na 2012.

Aidha katika taarifa hiyo Nalicho alidai kuwa endapo daraja hili la vyombo vya habari na wanahabari nkwa ujumla, endapo hawatatembelea huko na kuandika taarifa hizo watakuwa hawawatendei haki wananchi wa maeneo hayo hali ambayo itawafanya waendelee kulishwa taarifa za kupendelea wakati wote na kuwatetea viongozi ambao wapo maofisini.


Akifafanua taarifa haiyo mkuu wa wilaya hiyo, alisema kuwa mbali na juhudi za serikali kupeleka maendeleo kupitia sekta mbalimbali katika wilaya ya Tunduru lakini taarifa zake zimekuwa haziandikwi vya kutosha ikilinganishwa na maeneo mengine.

Alisema wilaya hiyo ambayo ipo pembezoni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za kutokuwa na barabara za uhakika zinazounganisha makao makuu ya wilaya na koa wa Ruvuma.

Vilevile imekuwa shida pia kuzifikia wilaya za Songea na Namtumbo mkoani wa Mtwara hali ambayo inazusha malalamiko mengi hasa nyakaati za masika.

Akizungumzia mapato ya ndani katika halmashauri ya wilaya hiyo Nalicho alisema kuwa katika kipindi hicho halmashauri ya wilaya hiyo imefanikiwa kuongeza hadi kufikia shilingi 718, 018,977 .43 kutoka shilingi 201,738,593.78 mwaka 2005 ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi 516,280,393.65.

Kuhusu sekta ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula alisema kuwa  katika kipindi hicho wilaya imeongeza kutoka tani 115,199 hadi tani 328,424 ikiwa ni ongezeko la asilimia 169.

Alisema hali hiyo imetokana na wilaya hiyo kuboresha miundombinu ya kujenga mifereji ya umwagiliaji. 

Pia kupeleka matrekta makubwa 25 kutoka 0 mwaka 2005, matrekta madogo (Powertillers) 187 na pembejeo za kilimo kutoka tani 900.65 mwaka 2005  hadi tani 6,412 mwak 2012.

Alisema upande wa sekta ya mifugo Nalicho alisema kuwa wilaya hiyo imepiga hatua kwa kuwa na ongezeko la Ng`ombe 35,758 kutoka 2,780 mwaka 2005, Mbuzi 43,413 kutoka 18,700, Nguruwe 3,110 kutoka 406 na Kuku 310,900 kutoka 107,430 hali ambayo imewasaidia wananchi wa wilaya ya Tunduru kuinua vipato vyao.

Akizungumzia changamoto mbalimbali na mikakati yake mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa vikwazo hivyo wilaya yake imekuwa ikijitahidi kukabiliana navyo ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango yakinifu ya kimaendeleo.      

No comments: