Diwani wa kata ya Mkumbi Bruno Kapinga(aliyevaa shati la kijani) akikabidhi msaada wa gunia la mihogo iliyomenywa na kukaushwa vizuri tayari kwa kusagwa na kupata unga wa kupika ugali, kwa mtoto mwenye ulemavu wa miguu na mgongo Elekta Kapinga, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Lugari katika kata hiyo. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wazee ambao nao walipatiwa msaada huo wa chakula. (Picha na Kassian Nyandindi)
Vilevile alisema ni vyema elimu itolewe katika jamii
ili kupunguza matatizo ya ukiukwaji wa haki za walemavu, wazee na watu
wasiojiweza ikiwemo kutowabagua katika maamuzi ya kifamilia.
Hata hivyo aliitaka jamii katika karne hii ya sayansi na teknolojia ibadilike na kuachana na mambo ya kiubaguzi kwa watu wenye hali hiyo badala yake watoe ushirikiano mkubwa katika kufanikisha maisha yao.
Na Kassian
Nyandindi,
Mbinga.
SERIKALI imetakiwa kuendelea kuelimisha jamii iwajali
na kuwaheshimu watu wenye ulemavu, wazee na watu wasiojiweza kama
walivyo watu wengine katika kupata haki sawa, ili waweze kusonga mbele
kimaendeleo na kuondokana na migogoro isiyo ya lazima miongoni mwa jamii.
Rai hiyo ilitolewa na Diwani wa kata ya Mkumbi
wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma Bruno Kapinga,
alipokuwa akitoa msaada wa chakula kwa watu wenye ulemavu, wazee na watu
wasiojiweza katika kata hiyo.
“Ndugu zangu hawa ni wenzetu ni lazima tuwajali katika
hata kuwapatia misaada mbalimbali, tukiwatenga tutakuwa tunakosea hivyo
tushirikiane pamoja”, alisema Kapinga.
Sambamba na hilo Kapinga ambaye pia ni Mjumbe wa
kamati ya chama cha mapinduzi(CCM) wilayani Mbinga, aliweza kutoa msaada wa
chakula ambacho ni mihogo iliyomenywa na kukaushwa vizuri tayari kwa kusagwa
kwa ajili ya kupata ugali.
Msaada huo ulitolewa kwa vijiji sita vilivyopo katika
kata ya Mkumbi, ambavyo ni Luwino, Longa, kipegei, Mkumbi, Lugari na Mtawa
ambapo jumla ya watu 300 walipatiwa msaada huo.
Hata hivyo aliitaka jamii katika karne hii ya sayansi na teknolojia ibadilike na kuachana na mambo ya kiubaguzi kwa watu wenye hali hiyo badala yake watoe ushirikiano mkubwa katika kufanikisha maisha yao.
No comments:
Post a Comment