Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
BARAZA
la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,
limemjia juu wakala wa barabara za mkoa huo(TANROAD) kwamba,
ameshindwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa barabara za wilaya hiyo, ambazo ujenzi
wake unasimamiwa na wakala huyo.
Licha
ya baraza hilo
kutoa malalamiko hayo kadhalika wameilalamikia TANROAD mkoani humo kwa kuwapa
tenda za ujenzi wa barabara za wilaya ya Mbinga, makandarasi ambao hawana sifa na vifaa vya
kutosha, ambavyo vingeweza kukidhi mahitaji halisi ya kujenga barabara kwa
kiwango kinachotakiwa.
Malalamiko
ya madiwani hao yalitolewa leo kwenye kikao cha kawaida cha baraza hilo, kilichoketi katika
ukumbi wa jumba la maendeleo uliopo Mbinga mjini.
Diwani
wa kata ya Litembo Altho Hyera alisema, aliweza kukutana na Meneja wa TANROAD
wa mkoa wa Ruvuma Abraham Kissimbo kuzungumzia suala hilo na kupewa majibu kwamba, barabara hizo
zinashinddwa kufikia viwango vya ubora unaotakiwa kutokana na kutotengewa fedha
za kutosha katika shughuli za ujenzi.
“Mheshimiwa
Mwenyekiti, kwa majibu ya meneja huyu haingii akilini, barabara za Tanroad
Mbinga zinaleta maswali mengi sana
hapa Mbinga, tunahitaji uwazi na ukweli katika hili”, alisema Hyera.
Aidha
pamoja na mambo mengine katika kikao hicho, Hyera alisema, ahadi iliyotolewa na
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2010,
juu ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kutoka Mbinga mjini hadi Litembo hospitali, haijatekelezwa hadi
sasa na muda unazidi kwenda na ni kwa sababu gani.
Akitolea
majibu juu ya suala hilo, Mbunge wa Mbinga
Mashariki Gaudence Kayombo alisema amekwisha lifikisha suala hilo katika vikao husika ngazi ya mkoa, hivyo
linafanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment