Na Steven Augustino,
Tunduru.
BARAZA la madiwani wa hlamashauri ya wilaya ya Tunduru
Ruvuma limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya matarajio ya kukusanya na
kutumia kiasio cha shilingi bilioni 34,425,566,350 katika kipindi cha mwaka 2013hadi 2014.
Akiwasilisha hivi karibuni taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Robert Nehatta katika kikao hicho
kilicho fanyika ukumbi wa Klasta mjini hapa, afisa mipango wa wilaya hiyo
Keneth Haule alisema kuwa kiasi hicho ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni
6,881,058,813 sawa na asilimia 19.9% ikilinganishwa na bajeti ya shilingi. bilioni
27,544,507,537 zilizo idhinishwa katika bajeti ya mwaka 2012 hadi 2013.
Akifafanua taarifa hiyo Bw. Haule alisema kuwa katika
ya fedha hizo Shilingi 34,425,566,350 zitatokana na makosanyo ya ndani vya
halmashauri hiyo,Ruzuku ya matumizi ya kawaida tsh.18,174,302,120 Mishahara shilingi 18,868,732,200 na matumizi mengineyo (PE) ni Tsh.2,237,201,000.
Taarifa hiyo iliyodaiwa huhitaji baraka za waheshimiwa
Madiwani wa wilaya ya Tunduru baada ya kupitiwa na kamati husika iliendelea
kufafanua kuwa kiasi cha shilingi 10,386,289,944 kitatokana na fedha za ruzuku
ya fedha za miradi ya maendeleo, pamoja na shilingi 310,716,000 fedha kutoka
katika mfuko wa kufidia vyanzo vya mapato vilivyofutwa (GPG).
Haule aliendelea kufafanua kuwa kati ya fedha hizo
halmashauri hiyo inatarajia kutumia shilingi 34,425,566,350 ambapo kati ya
fedha hizo shilingi 21,105,933,200 zimepangwa
kutumika katika matumizi ya kawaida.
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa kitengo cha mishahara
kwa watumishi zimepangwa shilingi 18,868,732,200 na kifungu cha matumizi
mengineyo kimepangiwa shilingi 2,237,201,000 huku miradi ya maendeleo
ikipangiwa shilingi 10,386,289,944.
Awali akifumgua na kufunga kikao hicho maalumu cha
baraza hilo Mwenyekitri wa halmashauri ya wilaya
hiyo Faridu Khamisi, aliwataka madiwani hao kutoa ushirikiano kwa watendaji,
ili kuwezesha halmashauri yao
kupiga hatua za maendeleo.
No comments:
Post a Comment