Na Steven Augustino,
Tunduru.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kuzima
tukio la ujambazi ambalo lilikuwa likifanywa katika mji wa Tunduru mkoni humo, kwa kutumia bunduki ya kivita aina ya SMG.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Deusdedit Nsemeki
alisema kuwa taarifa za kukamatwa kwa bunduki hiyo yenye namba 5637002531 zilifanikiwa
baada ya jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Alieleza kuwa bunduki hiyo bado haijajulikana inatoka
nchi gani, na kwamba imepatikana baada ya polisi kupata taarifa za
kiintelijensia, juu ya kuwepo mpango wa kufanyika tukio la ujambazi wilayani
Tunduru.
Alisema kufuatia taarifa hizo pia jeshi la polisi
lilifanikiwa kumnasa mtuhumiwa mmoja, aliyefahamika kwa jina la Jafar Hussein
Abdalah na kwamba hadi sasa yupo mikononi mwa polisi na sheria zitafuata mkondo
wake.
Kamanda Nsemeki alifafanua kuwa shughuli ya
bunduki hiyo iliyokamatwa aina ya SMG ilikutwa ikiwa imefichwa katika kijiji
cha Muungano mashambani.
Bunduki hiyo ya hatari ya tatu kukamatwa na polisi
mkoani Ruvuma, katika kipindi kisichozidi miezi sita iliyopita, tangu kamanda
huyo alipotangaza kutoa zawadi kwa mwananchi yeyote atakayefanikisha kupatikana
kwa bunduki zinazomilikiwa kinyume cha sheria.
“Hii ni bunduki ya tatu kukamatwa na polisi tangu
mwezi Septemba mwaka jana kwa bunduki za aina hii, alisema Kamanda Nsemeki na
kuongeza kuwa idadi hiyo haihusishi bunduki nyingine ndogo ndogo aina ya
Shortgun, Rifle pamoja na risasi zake.
Alisema mafanikio hayo yanatokana na utekelezaji wa
mpango wa polisi kwa kushirikiana na wananchi, kukamata silaha zote
zinazomilikiwa kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment