Rais Jakaya Kikwete. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
BARAZA la taifa la
hifadhi na usimamizi wa mazingira limeisimamisha kampuni ya Tancoal Energy,
inayochimba makaa ya mawe katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kufanya
kazi ya kupakia na kusafirisha makaa ya mawe katika kituo cha Amani
Makolo na Bandari ya Ndumbi, kwa muda wa siku saba kutokana na kukiuka
maagizo ya baraza hilo.
Kampuni hiyo
imesimamishwa baada ya timu ya baraza hilo la taifa la hifadhi na usimamizi wa
mazingira, kukagua na kutoa maelekezo mara kadhaa ya namna ya kupunguza athari
za vumbi kwa wananchi, uchafuzi wa vyanzo vya maji, kujenga vyoo na
mifereji ya kupitisha taka vimiminika na kampuni hiyo kutotekeleza maagizo hayo.
Dokta Madoshi
Makene alisema maeneo yaliyofungiwa kufanya kazi ni eneo la Amani Makolo
Mbinga na bandari ya Ndumbi, katika wilaya ya Nyasa mkoani humo, ambako
kunazalishwa kiasi kikubwa cha vumbi kutokana na shughuli ya upakiaji na
usafirishaji wa makaa hayo ya mawe na kushindwa kuzuia vumbi lisisambae katika
makazi ya watu.
Katika eneo
la Ndumbi timu hiyo haijakuta vyoo vilivyojengwa kwa ajili ya wafanyakazi, na
hakuna mifereji kwa ajili ya kupitisha maji machafu yanayotoka kwenye eneo hilo
ili yasiende kuchafua maji ya mito na ya ziwa Nyasa ambayo hutumika na wananchi
katika shughuli za maisha yao ya kila siku.
Kwa upande wao wakazi wa kijiji cha Amani makolo wilaya
ya Mbinga wanaomba serikali iwasaidie ili waweze kulipwa na kuhama, sasa wanashindwa
kuishi katika makazi yao kutokana na mazingira ya nyumba zao kuzungukwa na
vumbi na kusababisha watoto kuugua mafua na kikohozi.
Meneja wa
mazingira na usalama wa kampuni ya Tancoal Felix Fida, amekiri kuwa ni kweli
wanafahamu matatizo ya vumbi katika vituo hivyo, lakini kuna juhudi
zinazofanyika ili kupunguza ama kuondoa kabisa kero hiyo.
No comments:
Post a Comment