Msafara wa Mwenge wa Uhuru ukiwasili katika kijiji cha Liganga wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, tayari kwa makabidhiano ukitokea wilayani Mbinga. |
Mwenge wa Uhuru ukipelekwa katika eneo maalum, kwa ajili ya maandalizi ya kukabidhiwa wilaya ya Songea. |
Wanafunzi wa shule ya Msingi Liganga, wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe wa aina mbalimbali wa mbio za Mwenge wa Uhuru. |
Burudani ngoma za asili, nazo hazikuwa nyuma katika kijiji cha Liganga. |
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Juma Alli Simai, akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Liganga ambapo aliwasisitiza watoto hao, kuzingatia masomo wanapokuwa shuleni. |
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Juma Alli Simai, akiveshwa Skavu baada ya Mkuu wa wilaya ya Mbinga kumkabidhi kwa wananchi wa wilaya ya Songea. |
Senyi Ngaga Mkuu wa wilaya ya Mbinga, akitoa heshima(maelezo) kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya Songea. |
Tayari Mwenge wa Uhuru ukiwa katika eneo maalum, kwa ajili ya kuendelea na mbio zake wilayani Songea mkoa wa Ruvuma. (Picha zote na Kassian Nyandindi) |
Na Kassian Nyandindi,
Ruvuma.
HATIMAYE Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukiendelea kufanya kazi
zake wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, sasa umemaliza kazi husika salama na
kukabidhiwa leo kwa uongozi wa wilaya ya Songea.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika kijiji cha Liganga
wilayani humo, ambapo Mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga alifanya kazi ya
kumkabidhi kiongozi mwenzake ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph
Mkirikiti.
Wakati makabidhiano hayo yakifanyika kijijini hapo shamra shamra
na burudani za hapa na pale, zilikuwa zikiendelea kutolewa ambapo vikundi vya
ngoma za asili navyo havikuwa nyuma, katika makabidhiano hayo.
Kiongozi wa mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Juma Alli Simai naye hakuwa mbali katika kutoa
ujumbe wa mbio hizo, ikiwemo lile la kuwataka Watanzania kuendelea kuheshimu, kulinda
amani na utulivu huu tulionao.
Pamoja na mambo mengine Simai pia alisisitiza kwa wazazi
kuhakikisha watoto wao wanawapeleka shule, na sio kuwaacha majumbani.
Alisema jukumu la mzazi kumpeleka mtoto shule ni jambo la
lazima na sio hiari, hivyo linapaswa kuzingatiwa wakati wote kwa kuhakikisha pia
mtoto husika anapata mahitaji yake muhimu, awapo shuleni.
Mwenge wa Uhuru wilayani Mbinga, umeweza kufanya kazi kwenye
miradi 11 yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 1,061,881,200.
No comments:
Post a Comment