Kikundi cha Ngoma aina ya Mganda kikitumbuiza mara baada ya Mwenge wa Uhuru, kuwasili katika kijiji cha Mpapa wilayani Mbinga. |
Mwenge wa uhuru mara baada ya kuwasili ukitokea wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, ukipelekwa katika eneo maalum tayari kwa maandalizi ya makabidhiano kwa wilaya ya Mbinga mkoani humo. |
Mkuu wa wilaya ya Nyasa(Aliyeshika maiki) Ernest Kahindi, akizungumza, kutambulisha/kukabidhi wageni waliokuwa wakikimbiza Mwenge kwa ngazi ya kitaifa, mkoa na wilaya hiyo. |
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Juma Ally Simai akisalimiana na Mwenyekirti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbinga, Christantus Mbunda. |
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi, akijiandaa kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga. |
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akiupokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi. (Picha zote na Kassian Nyandindi) |
Na Kassian
Nyandindi,
Mbinga.
WATANZANIA wametakiwa kuwabeza, kuepukana na Viongozi wa dini
au siasa ambao hutumia majukwaa
kuhutubia wananchi, kwa nia ya kuchochea maneno yenye kujenga kuvuruga amani
iliyopo hapa nchini, badala yake wawe na mshikamano, upendo na utulivu ili
kuimarisha amani hiyo isiweze kuvurugika.
Rai hiyo iliotolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
Juma Ally Simai, alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge huo wakati akizungumza na baadhi
ya wananchi wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, katika kijiji cha Mpapa kata ya
Mpapa wilayani humo.
Simai alitoa kauli hiyo mara baada ya kumaliza kufanya makabidhiano
ya Mwenge huo kijijini hapo, ambapo awali msafara wa mwenge ulikuwa ukitokea
katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani humo.
“Ndugu zangu amani
ndio msingi mkuu wa maendeleo, kwa umoja wetu tulionao tuendelee kuudumisha
tuachane na mambo ya itikadi za kisiasa au dini, sisi sote ni wa moja”
“Tuepukane na viongozi wa dini au siasa wenye nia mbaya ya
kuvuruga umoja huu, taifa letu halikujengwa kwa misingi ya kiubaguzi”, alisisitiza
Simai.
Alieleza kuwa Tanzania ilipata Uhuru mapema, kutokana na
kuondoa ubaguzi miongozi mwa jamii.
“Amani ikitoweka ndani ya nchi madhara yake ni makubwa, hebu
angalia nchi za wenzetu ambao tunapakana nao, amani imevurugika hivyo
kuirudisha tena ni kazi kubwa sana”, alisema.
Pamoja na mambo mengine Mwenge wa Uhuru wilayani Mbinga
umeweza kufanya kazi kwenye miradi 11 yenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 1,061,881,200.
Katika miradi hiyo kazi iliyofanyika ni kuwekewa mawe ya
msingi, kufunguliwa, kuzinduliwa na kukaguliwa ambapo kati ya miradi hiyo nguvu
za Wananchi ni shilingi milioni 592,950,000 mchango wa Halmashauri 209,938,800
Serikali kuu 126,912,000 Wahisani 107,830,400 na nguvu za watu binafsi
24,250,000.
Hilo ni ongezeko la shilingi milioni 439,412,126 sawa na
asilimia 70.6 kwa miradi iliyotekelezwa wilayani Mbinga kwa mwaka jana (2012).
Hata hivyo Mwenge huo wa Uhuru leo Wananchi wa wilaya hiyo
wanakesha nao katika uwanja wa Taifa uliopo mjini hapa, na kuendelea na mbio
zake kesho, kuelekea wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
No comments:
Post a Comment