Washiriki wa kuchangia maoni ya rasimu ya katiba mpya wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Mbiku uliopo mjini hapa. |
Stevene Matteso akichangia hoja wakati wa kutoa maoni ya marekebisho ya rasimu ya katiba mpya katika ukumbi wa Mbiku uliopo mjini hapa. |
Walemavu nao hawakuwa mbali katika kusikiliza na kutoa maoni yao. (Picha zote na Kassian Nyandindi) |
Na Kassian
Nyandindi,
Mbinga.
WASHIRIKI katika uchangiaji wa maoni ya rasimu ya
katiba mpya wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, wametaka katiba ijayo ihakikishe
kwamba inaweka misingi ya kutambua makundi maalum, ikiwemo upatikanaji wa haki
zao bila kubaguliwa.
Pamoja na serikali kutoa matamko mengi juu ya haki za
Walemavu lakini utekelezaji wake umekuwa
hautekelezwi ipasavyo, jambo ambalo linasababisha kundi hilo likose haki zake
za msingi na kujikuta kutengwa na jamii.
Rai hiyo ilitolewa na washiriki hao ambao ni watu
wenye ulemavu wa aina mbalimbali wilayani Mbinga, wakati walipokuwa katika
mafunzo ya siku tatu ya katiba, ambayo yalifadhiliwa na shirika la The
foundation for civil society, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mbiku uliopo mjini
hapa.
Walisema kuwa haki za binadamu hususani kwa walemavu
zilizopo katika rasimu ya katiba mpya, haitambui ipasavyo watu hao kwa makundi
na mahitaji yao hivyo ni vyema yakafanyika mabadiliko ya dhati ikiwemo suala la
uhitaji wa vifaa vya kufundishia darasani hususani kwa watu wasioona na viziwi.
Mmoja kati ya washiriki hao aliyejitambulisha kwa jina
la Efigenia Kinunda alisema, hata Rais anapopewa nafasi ya kuteua watu kuingia
katika nafasi ya ubunge, katiba ijayo ihakikishe watu kutoka kwenye makundi
maalum, ni lazima nao wapewe kipaumbele katika kuwateua kwenye nafasi hiyo na
kwamba kila mkoa pawepo na mwakilishi wa nafasi ya ubunge ili kuweza kusaidia
kutambua kwa urahisi matatizo ya walemavu katika mkoa husika.
“Kwa ujumla rasimu hii ukiingalia kwa ujumla wake juu
haki za makundi maalum, inashindwa hata kuyatambua ipasavyo, tufike mahali
tukubali inatukandamiza kwa sehemu fulani”, alisema Kinunda.
Naye Steven Matteso alieleza kwamba katiba ijayo
ijenge mazingira ya kuwawezesha walemavu wawe wanapata matibabu bure, ruzuku
zitolewe kwenye vyama vya walemavu, kusamehewa kodi katika biashara
wanazozifanya na kuwepo miundombinu rafiki mashuleni na hata katika ofisi zinazohudumia
jamii.
Hata hivyo aliongeza kuwa katika katiba ijayo, itamke
kuwepo nafasi ya walemavu katika kuchangia uchumi wa nchi na haki sawa za
binadamu ikiwemo ajira katika sekta binafsi na serikalini.
No comments:
Post a Comment