Baadhi ya Wajumbe wakiangalia mahindi yaliyolimwa na kikundi cha Muungano kilichopo kata ya Kigonsera wilayani humo. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
WAJUMBE wa Jumuiya ya Serikali za mitaa (ALAT) mkoani Ruvuma
leo wameanza ziara ya kikazi kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani
Mbinga mkoani humo.
Aidha licha ya kutembelea miradi hiyo wanatarajia ifikapo
Aprili 23 mwaka huu, watafanya kikao chao kujadili maendeleo ya mkoa huo na
kuweka mikakati madhubuti ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, kwa faida ya
wananchi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Leo wakiwa katika ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani
Mbinga, wameweza kujionea shule ya Sekondari ya wasichana (Mbinga girls
Secondary school) iliyopo katika kata ya Kigonsera wilayani humo ambayo itaanza
kuchukua wanafunzi hivi karibuni.
Shule hiyo ni ya mchepuo wa masomo ya sayansi, inauwezo wa
kuchukua wanafunzi 80 watakaosoma hapo na wenye kipaji cha masomo hayo.
Kadhalika Wajumbe hao wa ALAT waliweza kutembelea na kujionea
shamba la mahindi kikundi cha Muungano, lililopo katika kijiji cha Kigonsera
lenye ekari 80 ambalo wanakikundi husika wameweza kulima mahindi kwa njia bora
za kisasa na ujenzi wa barabara kiwango cha lami kilometa moja Mbinga mjini, ambayo imekamilika.
Baada ya hapo kwa siku ya leo wameweza kuhitimisha ziara yao
kwa kushuhudia ujenzi wa Kituo kikuu cha kisasa, magari ya abiria ambacho kimejengwa
Mbinga mjini kinachotarajiwa kufanyiwa ufunguzi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Jakaya Kikwete, mapema mwezi Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment