Na Kassian Nyandindi,
Songea.
Songea.
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu
amesema, hakuna mtu atakayeweza kutengua maamuzi yaliyotolewa na serikali juu
ya kuvuliwa madaraka kwa aliyekuwa Ofisa elimu wa shule za sekondari wilayani
Mbinga, na Walimu wakuu sita wa shule hizo ambao walihusika katika matumizi
mabaya ya fedha za serikali.
Kauli hiyo ya Mwambungu ilifuatia Mwandishi wa habari hizi alipofanya
naye mahojiano juu ya malalamiko yaliyotolewa na Wadau wa elimu wa wilaya hiyo
kwa nyakati tofauti wilayani humo, baada ya kuona kumekuwa na njama
zinazofanyika chini kwa chini katika jitihada za kutaka kuwarejesha madarakani
watuhumiwa hao wanaodaiwa kutafuna fedha hizo.
“Hakuna anayeweza kufuta agizo hili lililotolewa na serikali hatua
zitachukuliwa na uamuzi utabaki palepale”, alisema Mwambungu.
Serikali mnamo
Februari 7 mwaka huu kupitia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi
ya waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Kassim Majaliwa,
alichukua hatua ya kumvua madaraka kwa kumshusha cheo aliyekuwa Ofisa elimu
Sekondari Hanji Yusuph Godigodi kwenda kuwa mwalimu wa kawaida akafundishe darasani na wenzake sita ambao ni walimu wakuu wa shule
za sekondari, kufuatia kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi na kufanya
ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 268 za maendeleo ya elimu ya sekondari
wilayani humo.
Wakuu wa shule za
sekondari wilayani Mbinga ambao walishushwa madaraka ni William Hyera ambaye ni
wa shule ya sekondari Maguu, Clemence Sangana anatoka shule ya sekondari
Mkuwani, Method Komba Langilo sekondari, John Tillia Ukilo sekondari, Leonard
Juma Luli Sekondari huku akimtaja kwa jina moja mwalimu Konga ambaye yupo
sekondari ya Kihangimahuka.
Fedha hizo zinazodaiwa
kutafunwa zililenga kufanya kazi ya kununua vitabu kwa shule za sekondari
wilayani Mbinga, lakini inashangaza kuona kwamba utekelezaji husika kama serikali ilivyopanga haukufanyika.
Katika fedha hizo shilingi milioni 108 ilibidi zitumike kununua vitabu hivyo, na zinazobakia zifanye shughuli nyingine za maendeleo husika katika shule hizo.
Katika fedha hizo shilingi milioni 108 ilibidi zitumike kununua vitabu hivyo, na zinazobakia zifanye shughuli nyingine za maendeleo husika katika shule hizo.
No comments:
Post a Comment