Na Kassian Nyandindi,
Nyasa.
ZOEZI la utoaji wa mashuka na vyandarua katika Hospitali ikiwa
ni lengo la kuwasaidia wagonjwa waweze kuwa na mazingira mazuri ya kulala pale
wanapolazwa wodini, leo limeendelea kufanyika wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma,
ambapo benki ya NMB hapa nchini kupitia tawi lake la Mbinga imetoa msaada huo wilayani humo.
Jumla ya mashuka 30, vyandarua nane
na foronya 30 vimetolewa na benki hiyo na kukabidhi kwa uongozi wa hospitali ya
wilaya hiyo huku makabidhiano hayo yakishuhudiwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Ernest
Kahindi.
Wilaya hiyo ambayo inakabiliwa na
changamoto lukuki katika sekta ya afya ikiwemo uhaba wa majengo ya kutolea huduma
hiyo muhimu vilevile magodoro, mashuka na mablanketi ya kulalia
wagonjwa zinahitajika jitihada za makusudi zifanyike kwa haraka ili kuweza kunusuru
hali hiyo.
Meneja wa NMB Kanda ya kusini
Lillian Mwinula akizungumza wakati wa kutoa msaada huo, aliushauri uongozi wa
wilaya ya Nyasa kuona namna ya kuandika maombi kwa benki hiyo ili waweze
kusaidiwa tena pale wanapoona wamekwama vifaa vya aina mbalimbali, ambavyo ni
muhimu katika kuhudumia wagonjwa.
“Benki yenu ya NMB ilianza na mtaji
kidogo sana, lakini kadiri siku na miaka inavyozidi kwenda mtaji umekuwa ukikua
na sehemu ya mtaji wake asilimia moja kila mwaka tumekuwa tukirudi kwa wananchi
na kuwasaidia kama hivi leo mnavyoona tumekuja hapa kwenu”, alisema Mwinula.
Alisema utaratibu huo unalenga
kuisaidia jamii yenye hali ya chini kimaisha, ili iweze kuondokana na adha
inayopata na hatimaye kusonga mbele kimaendeleo.
Pia Mwinula aliwataka Wananchi wa
wilaya ya Nyasa kuweka akiba katika benki hiyo, ikiwemo kuwafungulia akaunti
watoto wao ili waweze kujiendeleza kielimu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Kahindi aliushukuru uongozi wa benki hiyo kuona umuhimu wa kusaidia jamii, hususan katika maeneo ya kutolea huduma za afya na kuwataka waendeleze hilo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Awali benki hiyo ya NMB iliweza kutoa msaada wa Madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule ya msingi Komboa iliyopo kata ya Ruanda wilayani Mbinga.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Kahindi aliushukuru uongozi wa benki hiyo kuona umuhimu wa kusaidia jamii, hususan katika maeneo ya kutolea huduma za afya na kuwataka waendeleze hilo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Awali benki hiyo ya NMB iliweza kutoa msaada wa Madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule ya msingi Komboa iliyopo kata ya Ruanda wilayani Mbinga.
Sambamba na hilo pia ilitoa msaada wa mashuka 30 na vyandarua
10 katika hospitali ya wilaya hiyo, kwa ajili ya akina mama wajawazito ambao
husubiri siku ya kujifungua na kupata matibabu katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment