Na Steven Augustino,
Tunduru.
CHAMA cha Wananchi CUF Wilaya ya Tunduru mkoani
Ruvuma, kimewaomba wananchi wa wilaya hiyo kutotoa nafasi kwa viongozi watakaosimamishwa
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo.
Hayo yalibainishwa na Viongozi wa chama hicho wakati
wakizungumza katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya baraza
la Idd na kuongeza kuwa kauli hiyo wanaitoa kufuatia viongozi wa CCM waliopewa
dhamana na wananchi kushindwa kutimiza wajibu wao.
Mkurugenzi wa haki za bianadamu na sheria Mtukumbe Selemen Issa Ismail na Katibu wa CUF
wilaya Mchemela Salum Abudalah ni
miongoni mwa waliobainisha maelezo hayo, na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana
na viongozi waliopewa mamlaka hayo kutotimiza wajibu wao na kusababisha hata zao
la Korosho wilayani humo, wakulima kukosa soko la uhakika.
Walisema kutokana na hali hiyo hivi sasa wananchi wa wilaya
hiyo wanaishi maisha ya kukata tama, hali ambayo imewafanya washindwe hata
kupeleka watoto wao shule huku huduma ya chakula majumbani mwao, ikiwa ni shida.
Aidha katika hotuba hiyo pia viongozi hao wakagusia
makali ya maisha katika upatikanaji wa huduma za afya, kupanda kwa bidha ambako
walidai kuwa ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo.
Akihutubia kwa staili ya kulia huku akibubujikwa na
machozi mjumbe wa kamati ya siasa CUF wilaya ya Tunduru Said Kiosa alisema kuwa kinacho waponza na
kuwafanya wapatwe na madhila hayo, Wanatunduru ni tabia zao za upole na
kuridhika na kila linaloelezwa kuwa ni zuri kwao.
Kufuatia hali hiyo aliwataka wananchi hao kubadilika
na kutetea maendeleo yao, na ikishindikana iwe hata kwa kumwaga damu kama
walivyofanya wenzao wa wilaya za Masasi, Tandahima na Mtwara vinginevyo
wataendelea kubaki nyuma, huku mali zao zinaporwa na kuwanufaisha wajanja
wachache.
No comments:
Post a Comment