Mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
WADAU
wa michezo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma,
wamemuomba Mkuu wa wilaya hiyo Senyi Ngaga, kuingilia kati suala la kuinua
kiwango cha mpira wa miguu na mikono wilayani humo.
Vilevile
wadau hao walisema endapo mkuu huyo wa wilaya atafanya hivyo, wana hakika
kiwango cha mpira wilayani humo kitaenda vizuri, na kuifanya wilaya hiyo
wananchi wake waweze kupenda michezo.
Hayo
yalisemwa na wadau hao walipokuwa wakizungumza na mwandishi wetu, kwa nyakati
tofauti mjini hapa.
Walishauri
pia, katika kila msimu wa mavuno ya kahawa ni vyema ukaanzishwa utaratibu kwa
wafanyabiashara wanaonunua zao hilo
kuchangia kiasi kidogo cha fedha kwa kila kilo moja ya kahawa, ili fedha hizo
ziweze kutumika katika kuendeshea shughuli za mpira wa miguu kipindi ligi
mbalimbali zinapoendeshwa.
Walieleza
kuwa suala hilo ni vyema lifikishwe kwenye vikao
husika vya halmashauri ya wilaya hiyo ikiwemo Baraza la madiwani ili waweze
kutoa baraka zao na kuweka mikakati madhubuti ya kuweza kufanikiwa suala hilo.
Kadhalika
walieleza kuwa endapo suala hilo
litabarikiwa katika vikao hivyo, halmashauri ianzishe akaunti maalum ya michezo
ambayo itasimamia na kuweza kusaidia vilabu vya mpira wa miguu na mikono viweze
kusonga mbele.
Vilevile
waliongeza kuwa lengo la kufanya hivyo, itasaidia kuvifanya vilabu vya mpira
kutokuwa ombaomba na hatimaye kujiendesha vyenyewe.
No comments:
Post a Comment