Tunduru.
VIKONGWE
wa tano kutoka katika kijiji cha Mtonya wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma,
wamezuiliwa katika kituo kidogo cha polisi Nakapanya, ili kulinda usalama wa
maisha yao na kuwafanya wasishambuliwe kutokana na kutuhumiwa kufanya
ushirikina na kuwafundisha taaluma hiyo watoto wa watu bila ridhaa ya wazazi
wao.
Tukio
hilo lilitokea
baada ya vikongwe hao wanaodaiwa kuwa na uwezo wa kufungua na kuingia katika
nyumba za watu kwa njia za kishirikina, walifumwa wakifanya vitendo hivyo
katika kijiji cha Mindu wilayani humo.
Taarifa
zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nakapanya Kubodola
Ambali, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Spia Msusa (50), Ayana Iddi (75)
Adresia Maulid (68), Jenifer Saimon(60) na mwingine aliyefahamika kwa jina la
Biti Nyoya mwenye umri wa miaka 60.
Ambali
alifafanua kuwa mpango huo uligundulika baada ya wazazi wa mtoto Ally Milongo,
kuamka na kuanza kumtafuta mtoto wao mwenye umri wa miaka 10 kutoweka usiku wa
manane katika mazingira ya kutatanisha, ndani ya nyumba yao.
Baba
wa mtoto huyo Milongo Ally alisema kuwa baada ya tukio hilo la kutoweka kwa mtoto wake, yeye na mkewe
waliamka na kuanza kumtafuta katika maeneo tofauti ya kijiji hicho, ambapo
baadaye wakafanikiwa kuwaona wazee hao wakiwa uchi wa mnyama pamoja na kijana
wao, na walipojaribu kuwasogelea vikongwe hao walitoweka katika mazingira ya
kutatanisha.
Alisema
baada ya tukio hilo
walimkamata mtoto wao na kwenda naye nyumbani kwao, na baada ya kumbana na
kumtaka aeleze alikokuwa ndipo akawataja watu hao ambao baada ya kuitwa
walikiri na kuomba radhi kuwa hawatarudia tena, kumchukua mtoto huyo ambaye
walidai kuwa ni miongoni mwa washirika wao wa muda mrefu.
Alisema
katika tukio hilo
wazee hao walitozwa faini ya shilingi 100,000 ambayo waliilipa papo hapo, na
baadae wakaruhusiwa kuondoka.
Akiongelea
tukio hilo mtoto Ally Milongo alisema kuwa wakiwa mara kwa mara na
washirikina hao wamekuwa wakienda kumchukua yeye na watoto wenzake wane, na
kuwapeleka katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwafundisha utaalamu kuingia
na kuwachezea watu nyakati za usiku, na baadae hurejea majumbani kwao na
kufungua milango kwa kutumia matako huku wazazi wao wakiwa hawafahamu
kinachoendelea.
No comments:
Post a Comment