Na Steven Augustino,
Tunduru.
IMEBAINISHWA kuwa mahusiano mabaya kati ya Walimu na Wanafunzi ni moja kati ya kikwazo kilichoelezwa kwamba huchangia kuzorota kwa elimu wilayani humo.
Kadhalika wanafunzi kukataa kukaa katika mabweni au hosteli
ni miongoni mwa vikwazo vya maendeleo ya elimu wilayani Tunduru na kusababisha
wilaya hiyo kupata matokeo mabaya kwa wanafunzi waliofanya mitihani ya kidato
cha pili na nne katika kipindi cha mwaka 2011/2012.
Hayo yalibainishwa na afisa elimu
sekondari Ally Mtamila wakati akiwasilisha taarifa yake ya matokeo ya kidato
cha pili na cha nne katika kipindi cha mwaka 2011/2012 katika mkutano maalum
ulioketi wilayani humo, na kuongeza kwa kuwataka wazazi kushiriki kikamilifu katika
usimamiaji wa watoto wao ili waweze kuwa na hamasa ya kupenda masomo wanapokuwa
shuleni au nyumbani.
Vilevile wazazi kukemea watoto wanaokwepa
kuingia darasani ambao wamekuwa wakiachwa waendelee kucheza wakati wenzao
wakiwa darasani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mwaka
2011 matokeo ya kidato cha pili wilaya hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia
35%, huku takwimu hizo kwa upande wa matokeo ya kidato cha nne katika kipindi
cha mwaka 2012 zikionesha kuwa wilaya, ilifaulisha kwa wastani wa asilimia
59.46% kiwango kilichodaiwa kuwa ni kidogo na kiliifanya kushika nafasi ya
mwisho kimkoa.
Awali akifungua mkutano mkuu wa wilaya
ya Tunduru Chande Nalicho pamoja na kubainisha kuwa serikali kuwa na
vipaumbele vingine vya maendeleo lakini elimu ni muhimu kwa kile alichoeleza
kwamba ndio msingi wa maisha.
Nalicho alieleza kuwa ili kuwaletea
maendeleo wananchi wa Tunduru, ni lazima wilaya ijikite katika kusimamia elimu kwanza
mambo mengine yafuate baadaye.
Katika taarifa hiyo mkuu huyo wa
wilaya, alitolea mfano wa takwimu za ufaulu wanafunzi 2764 waliochaguliwa
kujiunga na masomo ya sekondari hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu, ni
asilimia 60% ya watoto wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya
sekondari.
Akizungumzia upande wa shule za msingi
mwaka 2011shule ya msingi Nakapanya wilayani humo, ilifaulisha watoto 26 lakini
takwimu zinaonesha kuwa watoto wote hawakwenda shule na kuongeza kuwa,
hali hiyo inawakatisha tamaa walimu wa shule za msingi zinazoendele kufaulisha
watoto.
Wakichangia kwa nyakati tofauti mwalimu
Issa Ngajime alisema kuwa chanzo cha kushamiri kwa utoro, uchangiaji hafifu wa
chakula mashuleni na wanafunzi kukataa kukaa katika hostel zilizojengwa katika
shule zao, viongozi wa serikali za vijiji wanastahili kubeba lawama, huku wakiwataka
viongozi kutochanganya elimu na siasa.
Aidha mbinu za kufundishia
imeshauriwa kuendelea kuboresha na kuchukua hatua kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakibainika
kuchaguliwa wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
Mkuu wa shule ya Mgomba Elis Banda
alisema kuwa tatizo la wanafunzi kukataa kukaa katika hosteli, linatokana na
kuwepo kwa idadi kubwa ya watoto wanaosoma katika shule hizo kuwa ni wakazi wa
maeneo husika na akapendekekeza kuwepo kwa utaratibu wa kutenga shule za kanda
kwa ajili ya kupeleka wanafunzi kutoka maeneo tofauti, huku akiitaka serikali
kutoa maelekezo ya vitabu vya kununua tofauti na sasa ambapo kumekuwa na
maelekezo ya kuwataka wakuu wa shule kutumia vitabu kutoka katika kampuni ya
EMACK.
Wanafunzi kupewa mamba imekuwa
nalko ni tatizo lakini bodi za shule zimekuwa zikifanya kazi ya ziada kudhibiti
hili, lakini kila wanapofuatilia matokeo ya kesi polisi huwa
hawapatiwi majibu ya maendeleo ya kesi husika hali inayo wakosesha imani kuwa huenda kesi hizo zimekuwa zikipeleka ulaji kwa jeshi hilo.
hawapatiwi majibu ya maendeleo ya kesi husika hali inayo wakosesha imani kuwa huenda kesi hizo zimekuwa zikipeleka ulaji kwa jeshi hilo.
Mkuu wa shule ya sekondari
Lukumbule Mathias Katto akabainisha vikwazo vingine kuwa shule zao kutokuwa na
walimu wa masomo ya Sayansi, kutokuwa na maktaba na nyumba za walimu kutokuwa
bora ni kikwazo kimojawapo.
Marafiki hao wa elimu pia
wakanyooshea kidole mila na desturi potofu za kuwafundisha watoto wadogo, hasa
wakike mafunzo ya kuishi kinyumba ambayo hutolewa kupitia mafunzo katika jando, Unyago na Msondo na ngoma ya
Sakamimba hali ambayo imekuwa ikipelekea baadhi ya wanafunzi, kuishi kwa
wanaume huku wakiwa wanaendelea na masomo.
No comments:
Post a Comment