Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu. |
Na Steven Augustino,
Tunduru.
MKUU
wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Chande
Nalicho amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo,
kuwachukua hatua ikibidi hata kuwafukuza kazi, watumishi wasiowajibika ikiwa ni
juhudi za serikali kuinua taaluma wilayani humo.
Nalicho
alisema hayo wakati akifunga mkutano wa kutathimini matokeo kidato cha pili, nne
na sita uliofanyika katika ukumbi wa klasta Mjini humo na kuongeza kuwa hali
hiyo imetokana na serikali kubaini kuwa watumishi wa kada zote wilayani
humo, hawako tayari kufanya kazi kwa kujituma hali iliyopelekea wilaya hiyo
kuwa nyuma kielimu.
“Viongozi
ndio wasiopenda kufanya kazi, wamebakia kula mishahara tu na ndiyo maana katika
wilaya hii, tumeendelea kuwa nyuma kielimu”, alisema Nalicho na kuongeza kwa
kumtaka mkurugenzi awachukulie hatua za kinidhamu.
Alisema
inashangaza kuona kuwa Tunduru ikiwa imekithiri kwa utoro wa wanafunzi lakini
inapotokea ofisi yake inahitaji taarifa za matukio hayo maafisa tarafa, watendaji
wa kata na viongozi wa vijiji wengi wanapoulizwa juu ya idadi ya wanafunzi
waliofaulu na kucahaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari wanadai kutokuwa na
takwimu zake.
Nalicho
aliendelea kubainisha viashiria vingine vya viongozi hao kutowajibika kuwa ni
pamoja na kuwepo kwa takwimu kubwa za utoro ambazo hazifanyiwi kazi, amnapo alitolea mfano
shule ya msingi Njenga ambayo takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2010 ilifaulisha
wanafunzi 41 waliokwenda shule walikuwa 3 mwaka 2011 walifaulu 46 walioendelea
na masomo 7 na mwaka 2012 walifaulu 17 waliokwenda shule hadi sasa 1.
Naye
Mwenyekiti wa huduma za jamii Diwani Athumani Nkinde pamoja na kukiri kuwa zipo
shule za sekondari ambazo zilijengwa kisiasa na kutolea mfano shule ya
sekondari Nampungu, ambayo inaonesha kutelekezwa na wananchi kwa kutopeleka
wanafunzi alipigilia msumali wa moto kwa kuzitaka mamlaka husika kuchukua hatua
za kisheria, kwa wanafunzi na wazazi wao ambao hawakupeleka watoto katrika
shule hiyo.
Akizungumzia
mikakati ya kuinua taaluma na kuiondoa idara yake katika kashfa hii ya kupeleka
sekondari wanafunzi wasiojua kuandika, kusoma na kuhesabu kaimu afisa elimu wa
shule za msingi Flavian Nchimbi alisema kuwa wilaya inaendelea kujidhatiti kwa
kutumia mitihani ya majaribio katika kata pamoja na kuendesha mafunzo ya mada
ngumu kwa walimu ikiwa ni juhudi ya kuinua taaluma kwa wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment