Na Mwandishi wetu,
WANAWAKE pamoja na watoto wa kike wa mkoa wa Shinyanga Jimbo la
Kishapu kata ya Mnhunze nchini Tanzania wanakabiliwa na matatizo ya
kubakwa na kupigwa, kwa sababu ya shida ya maji.
Mbali na matukio hayo pia wamekuwa wahanga wa kupigwa na waume zao
baada ya kuchelewa kurudi jumbani kutokana na kwenda umbali mrefu
kutafuta maji.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wanawake
wa vijiji vya Mnhunze, Kisoso na Lubago wamesema kwamba mateso hayo pia
wanakabiliwa na mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kwa sababu ya kutumia
maji yasiyostahili kwa matumizi ya binadamu ili kuepuakana na shida
matatizo hayo hayo.
"Tunalazimika kuamka saa tisa za
usiku kutafuta maji baada ya tatizo hili kuzungumziwa mara kwa mara
bila mafanikio yoyote yanayoonekana"alisema Anastazia Christopher mkazi wa kijiji cha Isoso.
Paskazia John mkazi wa kijiji cha Lubaga katika kata ya Mnhunze
alielezea machungu anayoyapata juu ya janga hilo kubwa la maji
linalowakabili wakazi wa kijiji chao na kudai kwamba linamnyima raha
kutokana na baada ya kuwa chanzo cha kuleta matatizo ya kifamilia
katika jamii yao.
"Mambo mengi sana yanatokea kutokana na tatizo hili la ukosefu wa
maji kwani maji yanapatikana mbali sana na inawalazimu kuamka saa tisa
usiku ili waweze kuyapata maji,pia imesababisha madhara makubwa sana kwa
watoto wao wa kike", alisema John.
No comments:
Post a Comment