Editruda Mashimi,
Dar es Salaam.
RASIMU ya Katiba mpya inayoruhusu
muundo wa serikali tatu imezidi kukichanganya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Chama hicho tawala kimepinga muundo huo kimesema bado kinaamini katika
muundo wa Serikali mbili.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma jana, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia kwamba mapendekezo
yaliyofikishwa mbele ya tume hiyo yatabaki kama yalivyo,Na hivyo msimamo
wao ni kuwepo kwa muungano wenye Serikali mbili kama ilivyo sasa.
“Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye
Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali mbili na siyo tatu wala
moja,” alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu
(CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.
Wakati CCM ikipinga kuwepo kwa
serikali tatu, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chakawe amesema upo
uwezekazo wa Katiba Mpya ya Tanzania Bara ikapatikana kabla ya Uchaguzi
Mkuu wa 2015.
Chikawe alisema kwamba
ikiwa mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama
inavyokusudiwa na rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote
bila mabadiliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya Tanzania
Bara.
“Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila
mabadiliko na kupata Katiba Mpya. April mwakani mpaka Desemba inatosha
kabisa kuandaa Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu
tukiwa na Katiba Mpya,” alisema Chikawe.
No comments:
Post a Comment