Wachezaji wa mpira wa pete, wakiendelea kuonesha vipaji vyao uwanja wa michezo Mbinga mjini. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
LIGI ya Nanenane ya
mpira wa pete wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ikiwa inaendelea kwa kasi
mjini hapa kutimua vumbi, timu mbili zimeonyesha kiwango chake cha mchezo
kwenye uwanja wa michezo Mbinga mjini.
Timu ya Chuo cha
Maendeleo ya Jamii [FDC] ndiyo ambayo ilikuwa ya kwanza kufungua dimba majira
ya saa 8:00 mchana ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 28-4 dhidi ya Timu ya
Nyoni.
Katika kipindi chote
cha mchezo huo timu ya Nyoni ilionekana kuwa machachali kimchezo, lakini
hadi mwisho haikuweza kuzaa matunda na ilionekana ikiwa nyuma kimagoli.
Aidha timu nyingine
katika mashindano hayo ambayo ilianza kucheza majira ya saa 9:30 alasiri,
Polisi ya mjini hapa iliibuka na ushindi wa mabao 15 - 5 dhidi ya wapinzani wao
Bambo Invenstment ya Myangayanga.
Katika mchezo huo timu
zote mbili zilionekana zikiwa na nguvu sawa katika kipindi cha kwanza na
kwamba timu ya Bambo Invenstment ya Myangayanga, imeonekana kuwa ikichezesha vijana
wenye umri mdogo na ambayo inanizamu kimchezo zaidi kuliko timu nyingine
zote zinazoshiriki mashindano hayo, ambapo refalii Winfrida Amlani hadi alipopuliza
kipenga chake cha mwisho kila timu iliibuka na ushindi wake.
Kwa upande wa kocha
msaidizi wa timu ya Polisi na Bambo invenstment, Mariamu Honde aliziambia
timu zake kuwa zinauhakika wa kuchukua ushindi, kwa kuwa timu hizo zinaongoza
kimagoli, na kwamba wanahitaji walimu tu wa kufundisha michezo hiyo hasa timu
za vijijini ambazo zimeonekana kuwa nyuma sana kimchezo, na kushindwa kufuata
utaratibu na kanuni husika, kuliko timu nyingine ambazo zinashiriki
mashindano hayo.
Hata hivyo Honde
aliitaka serikali wilayani hapa itoe mafuzo ya makocha wa mpira wa pete,
kwa kuwa mchezo huo umeonekana kuwa nyuma kuliko michezo mingine ambayo
inachezwa katika wilaya ya Mbinga.
No comments:
Post a Comment